WAANDISHI WA HABARI WAKIHAHA KUJIKOSHA NA MAJI MARA BAADA YA POLISI KURUSHA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIFANYA FUJO KATIKA ENEO LA OFISI ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA JANA JIONI.
AKISIMAMA JUU KATIKA NGUZO ZA GETI KUU OFISI ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KIJANA HUYU ALIKUWA AKILIA KWA MACHUNGU KWA NINI MATOKEO YANACHELEWA KUTANGAZWA.
MGOMBEA UBUNGE WILAYA YA NAYMAGANA BW. WENJWE AKIWATULIZA WANACHAMA WAKE KUWA WATULIVU NA KUYASUBIRI MATOKEO RASMI MARA BAADA YA UHAKIKI KUFANYIKA INGAWA TAYARI KULIKUWA NA DALILI ZA WATU KUCHOKA KUYASUBIRI MATOKEO HAPA ILIKUWA SAA NANE NA DK 45 MCHANA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SIMON SIRO ALIWASIHI WANANCHI KUWA WATULIVU NA KUTOFANYA VURUGU KWANI JESHI HILO LIKO MAHALI HAPO KULINDA AMANI NA USALAMA HUKU LIKI HAKIKISHA ZOEZI HILO KUWA LINAFANYIKA KWA HAKI NA WANANCHI KUSHEREHEKEA USHINDI WAO KWA AMANI.
WATU MAELFU KWA MAELFU KUTOKA KATA ZOTE ZA WILAYA ZOTE MBILI (NYAMAGANA NA ILEMELA) WALIANDAMANA KUFIKA KATIKA OFISI HIZO KUSIKILIZA MATOKEO.
SHUGHULI NDANI YA SHUGHULI.
MAANDAMANO TOKA IGOMA YAKIWASILI ENEO HILO.
HALI JINSI ILIVYOKUWA KWA SIKU YA JANA HATUA KWA HATUA MASAA YAKIYOYOMA.
KAZI ILIKUWA NZITO KADRI MUDA UKISONGA HUKU WANANCHI WAKIONGEZEKA ENEO LA TUKIO, ULINZI NAO UKIIMARISHWA.
MOJA YA ATHARI ZILIZOJITOKEZA NI KUCHOMWA MOTO KWA OFISI ZA CCM KITUO CHA NELA NA KUTEKETEA KABISA ZIMAMOTO IKISHINDWA KUFIKA ENEO HILO KUTOKANA NA VURUGU NA MAWE MAKUBWA YALIYOTANDAZWA BARABARANI.
WANANCHI HAO WALIANZA KURUSHA MAWE KTK OFISI HIZO ZA JIJI NA HATIMAYE WAKAVUNJA UPANDE MMOJA WA KUSHIKILIA GETI KUU LA KUINGIA OFISI HIZO HALI ILIYOSABABISHA GETI KUKOSA BALANCE HIVYO WAO KUPENYA KIRAHISI NA KUKARIBIA ENEO LA TUKIO.
WAKIWA WANAJUA DHAHIRI NANI WASHINDI NA KAPATA KURA NGAPI WAFUASI HAO WALIANZA KUIMBA KWAMBA ‘TUNASIKIA HARUFU YA DAMU’ NA HATA KUDIRIKI KUMSHUTUMU MGOMBEA WAO BWANA WENJE WAKIDAI KUWA KAPEWA RUSHA NA KUWAGEUKA NDIYO MANA ALIWATULIZA WANACHAMA WAKE KUSUBIRI MATOKEO AMBAYO YALIYODAIWA YANGETOKA BAADA YA MUDA WA SAA 1 NA NUSU NA YASITOKE. PONGEZI KWA JESHI LA POLISI KWA UVUMILIVU WAO KUPOKEA KEJELI NA KUMWAGIWA MIKOJO BILA KUCHUKUWA HATUA ZOZOTE, WALINZI HAO WALIPATA WAKATI MGUMU KUJIBU HOJA ZA MADHAIFU YA WENGINE.
KATIKA OFISI HIZO AMBAPO ILIKUWA HAKUNA KUTOKA WALA KUINGIA. JESHI LA POLISI LILITUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATULIZA WAFUASI HAO LAKINI WAPI SHUGHULI ILIKUWA NGUMU.
VURUGU ZILIKOLEA NA KUTISHA AMBAPO MOJA YA GARI LILILOKUWA LIMEPAKI NJE YA OFISI HIZO LILICHOMWA MOTO NA MENGINE ZAIDI YA KUMI KUVUNJWA VIOO.
MOJA YA MAGARI OFISINI HAPO YALIYODHURIKA.
GARI JINGINE LILILOPAKI ENEO LA NDANI NYUMA YA OFISI HIZO AMBAPO ILIBIDI KWA KIPINDI KIFUPI WATU WALIKUWA WAKIHAHA KUTOKA ENEO LA TIMBWILI WAJUE RAMANI YA JENGO ZIMA.
MAWE MAKUBWA AMBAYO WAWEZA KUJIULIZA YALIWEZAJE KUFIKA BARABARANI YALIPANGWA BARABARANI KUTORUHUSU MAGARI KUPITA YALIPANGWA BARABARANI KUTORUHUSU MAGARI KUPITA KATIKA NJIA ZOTE KUU. PICHANI MOJA YA VIJIKO VIKIONDOA MAWE HAYO LEO ASUBUHI.
HALI YA VURUGU ILITULIA MAJIRA YA SAA 1USIKU MARA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA NAE MSIMAMIZI WA UCHAGUZI MWANZA AMBAYE PIA NI MKURUGENZI WA JIJI BW. WILSON KABWE. NYAMAGANA UBUNGE UMEKWENDA KWA BW. WENJE WA CHADEMA ALIYEPATA KURA 38,871 AKIMWANGUSHA BW.LAU MASHA ALIYEPATA KURA 27,883 KURA ZILIZOPIGWA ZILIKUWA 67,560 WALIOJIANDIKISHA 189,976. KWA UPANDE WA ILEMELA MGOMBEA WA CHADEMA BW. HAINES SAMSON (KURA 31,296)AMEMBWAGA ANTHONY DIALO WA CCM (KURA 26,870). PICHANI HALI YA HEWA LEO ASUBUHI.
Tupe maoni yako
Helo, Jimbo la Karagwe, jioni hii yametokea yale yale. Watu wamemwagiwa maji yanayowasha na gari la FFU na mabomu ya machozi kupigwa. Kisa? Matokeo jamaa muhusika amekataa kuyatangaza. Je, tutafika?
ReplyDeleteNimewakubali sana watu wangu wa mwanza, hawa ndio wajanja wa tz na sio wale wa dar
ReplyDeletempaka kielweke na kimeeleweka