MRATIBU WA MASHINDANO HAYO GERLARD NDIMILA AMESEMA MASHINDANO HAYO YATAHUSISHA WILAYA 4 AMBAPO MBILI NI KUTOKA MKOA WA MWANZA NA MBILI KUTOKA MKOA WA SHINYANGA, MKOA WA MWANZA NI WILAYA YA NYAMAGANA NA GEITA NAKO SHINYANGA NI WILAYA ZA KAHAMA NA SHY TOWN.
MASHINDANO HAYO YA MTOANO YA DUME CUP YATAKAYO FANYIKA KATIKA WILAYA HIZO TAJWA YAMELENGA KUZISHIRIKISHA TIMU ZA WAVUVI, WAFANYAKAZI WA MIGODI, WAUZA MITUMBA, MAGAZETI, WAPIGADEBE NA WASUKUMAJI MIKOKOTENI.
NAYE MJUMBE WA KAMATI YA CHAMA CHA SOKA MKOANI MWANZA (MZFA) MUTANI YANGWE AMEONGEZA KWA KUSEMA KUWA MASHINDANO HAYO YANAYOTARAJI KUANZA KUSHIKA KASI KUANZIA TAREHE 8,OCTOBER 2010 YATAENDESHWA KWA KUTUMIA SHERIA NA KANUNI ZA SOKA ULIMWENGUNI FIFA NA KUSIMAMIWA NA WAAMUZI WENYE VIWANGO WANAO TAMBULIWA NA TFF.
SAMBAMBA NA VIKOMBE KWA MSHINDI WA KWANZA NA WAPILI ZAWADI NYINGINE KWA KWA MSHINDI WA KWANZA NI DUME LA NG’OMBE NA MBUZI WAWILI HUKU MSHINDI WA PILI AKIKAMATA KIKOMBE NA MBUZI MMOJA HUKU WASHIRIKI WALIOSALIA KUZAWADIWA T-SHIRT ZILIZOBEBA UJUMBE WA KUHAMASISHA MCHAKATO MZIMA.
SHIRIKA LA T-MARC KUPITIA DUME CUP PAMOJA NA KUTUMIA MASHINDANO HAYO KUCHUNGUZA NA KUFANYA TATHMINI YA JUU YA ELIMU ITOTOLEWAYO KAMA INAFIKA IPASAVYO VILEVILE SHIRIKA HILO LITATUMIA NAFASI HIYO KUTOA TENA NA TENA ELIMU YA MATUMIZI YA CONDOM IKIWA NI MCHANGO WAKE KWA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI.
UDHAMINI WA DUME KATIKA MASHINDANO HAYO (DUME CUP) UMELENGA MAENEO YENYE MAAMBUKIZI MAKUBWA YA VIRUSI VYA UKIMWI, SEHEMU ZA BIASHARA, BIASHARA YA USAFIRI, KILIMO CHA BIASHARA, MACHIMBO YA MADINI NA BIASHARA YA UVUVI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.