ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 26, 2009

HOMA YA MAFUA YA NGURUWE YAINGIA MWANZA




WAKATI TAIFA LA TANZANIA LIKIENDELEA KUJIPANGA NA KUJIZATITI KATIKA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA HOMA KALI YA MAFUA YA NGURUWE MKOA WA MWANZA UMETHIBITISHA KUINGILIWA NA UGONJWA HUO HATARI.
AKIZUNGUMZA LEO HII OFISINI KWAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA DR.MESHARK MASSI AMESEMA KUWA UGONJWA HUO AWALI ULIGUNDULIKA KATIKA KIJIJI ILULA WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA AMBAPO WANAFUNZI 56 WA SHULE YA MSINGI ILULA WALIONEKANA KUWA NA DALILI MBALIMBALI ZA UGONJWA HUO.
MARA BAADA YA HAPO IDARA YAKE YA AFYA WILAYA ILITUMA TIMU YA WATAALAMU KUCHUNGUZA HALI, KUPATA VIPIMO NA SAMPULI NDIPO MAJIBU YAMETOKA HII LEO KUBAINISHA KUWA JUMLA YA WATU 142 WAMEATHIRIKI NA UGONJWA HUO IKIWA NI WANAFUNZI, WAALIMU NA BAADHI YA WANAKIJIJI WA ILULA WILAYANI KWIMBA.
KATIKA HALI HIYO MGANGA MKUU HUYO WA MKOA WA MWANZA AMETOA WITO KWA WANANCHI WA KIJIJI HICHO NA VIJIJI JIRANI KUCHUKUA TAHADHARI ZINAZOSTAHILI KUJIKINGA NA MARADHI HAYO IKIWA NI PAMOJA NA KUNAWA MIKONO KWA SABUNI NA MAJI SAFI MARA KWA MARA, VILEVILE KUEPUKA KUWA KUWA KARIBU NA MTU MWENYE DALILI ZA UGONJWA HUO
AIDHA DR. MASSI AMEWAASA WANANCHI KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA LAINI / TISSUE WAKATI WA KUKOHOA NA KUPIGA CHAFYA, KUFUATA KANUNI ZOTE ZA AFYA NA KWA WAFUGA NGURUWE KUZINGATIA DALILI ZA UGONJWA KWA NGURUWE NA KUEPUKA KUGUSANA NA MIFUGO HIYO IWAPO ITAONEKANA KUWA NA DALILI ZINAZOTAJWA NA WAELIMISHAJI.
SHANGWE LILILIPUKA TOKA KWA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA MGANGA MKUU HUYO KUNENA KWAMBA "UGONJWA WA MAFUA YA NGURUWE HAUAMBUKIZWI KWA KULA NYAMA YA NGURUWE ILIYOPIKWA" HATA RAFIKI YANGU ..... ALISHANGILIA. HATA HIVYO INATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WA MAANDALIZI NA KABLA NYAMA HAIJAPIKWA.
MPAKA SASA HAKUNA TAARIFA ZOZOTE ZA MGONJWA WA MARADHI YA MAFUA YA NGURUWE ALIYERIPOTIWA KUFARIKI DUNIA MKOANI MWANZA.
SHULE YA ILULA IMEFUNGWA TANGU TAREHE 19 NOVEMBER 2009 MARA TU BAADA YA WANAFUNZI WA SHULE HIYO KUGUNDULIKA KUWA NA DALILI ZA UGONJWA HUO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.