ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 11, 2009

DECI NYINGINE YAPIGWA STOP

SERIKALI WILAYANI BUNDA MKOANI MARA IMEAGIZA KAMPUNI MOJA INAYODAI KUSAIDIA WANANCHI MISAADA MBALIMBALI BAADA YA KUCHANGIA FEDHA ZAO, IKIWEMO KUSOMESHA WATOTO HADI ELIMU YA JUU NA KUWAJENGEA NYUMBA NA SHULE WANACHAMA WAKE, KUACHA MARA MOJA SHUGHULI ZAKE MPAKA HAPO ITAKAPOKUWA IMEJIRIDHISHA KAMA SIYO YA KITAPELI.
+ AGLZO HILO LIMETOLEWA JUZI NA KATIBU TAWALA (DAS) WA WILAYA YA BUNDA, DEO MANGAZENI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAWAKILISHI WA ASASI NA MASHIRIKA YASIYOKUWA YA KISERIKALI MJINI BUNDA.
+ KAMPUNI ILIYOPIGWA STOP NA SERIKALI INAJULIKANA KWA JINA LA PEOPLES UNITY FOR DEVELOPMENT IN AFRICA (PUFDIA) INAYOFADHILIWA NA MTANDAO WA KIKRISTO DUNIANI CHINI YA BW. TURKO SIMON WA MAREKANI.
+ KAMPUNI HIYO INAYODAIWA KUSAIDIA WANANCHI KWA MASHARTI NAFUU ILI WAONDOKANE NA UMASKINI KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO CHA FEDHA TAYARI ILIKUWA IMEPATA OFISI NA KUANZA KUTOA MATANGAZO KWA NJIA YA KIPAZA SAUTI NA VIPEPERUSHI.
+MOJA KATI YA VIPENGELE VILIVYOMO KWENYE VIPEPERUSHI HIVYO VINASEMA := ILI MWANANCHI AJENGEWE NYUMBA ANATAKIWA KUTOA KUPANDA KIASI CHA SH 470,000 TU.
++ KAA CHINI TAFAKARI++

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.