Kuna vitu vitatu ambavyo Raila alikuwa akivililia
1. Server ya matokeo ya uchaguzi uliopita ifunguliwe ili wapate kujua matokeo halisi. 2. Usawa katika muundo wa Tume ya uchaguzi Kenya #IEBC. 3. Mfumuko wa bei ya vyakula unaosababisha ukali wa maisha. Lakini inasemekana mpaka mazungumzo ya siri yanafanyika baina ya kiongozi wa #Azimio , Raila Odinga na Rais William Ruto hakuna mwanga wa muafaka ulioonekana kuelekea majibu ya maswali hayo, hivyo wameapa kurudi tena barabarani kwa maandamano kuanzia kesho jumatatu na Raila kesha tangaza kwa wafuasi wake. #uchaguzikenyaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.