ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 9, 2023

"KIONGOZI MPENDA AMANI" RAILA AWAOMBA WAKENYA KUIGA MFANO WA YESU KATIKA UJUMBE WAKE WA PASAKA


Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga sasa anawataka Wakenya kuiga mfano wa Yesu Kristo wakati huu wa likizo ya Pasaka.

Katika ujumbe wake wa Pasaka kwa Wakenya kupitia kwenye mitandao ya kijamii, Raila aliwataka Wakenya kuganda na mafunzo ya Yesu msimu huu na Pasaka zingine zijazo.

"Ninatumahi kuwa hii Pasaka na nyingi zitakazofuata, tunaweza kujifungza kutumia fursa jinsi Yesu alivyofanya. Ni tumaini langu pia tunaweza kuendelea kujiahidi kufuata yale ambayo Yesu alihubiri," Raila alisema. 

Kiongozi huyo wa chama cha ODM alifupisha mafundisho ya Yesu, miongoni mwayo ujasiri, upendo, amani, uvumulivu na kuwa na matumaini. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.