Maafisa Tarafa na watendaji wa kata zote za wilaya ya Iringa wameahidi kuwa mabalozi wa kuvitangaza vivitio vya utalii vilivyopo katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ili kuongeza chachu ya ongezeko la watalii katika ukanda wa nyanda za juu kusini ikiwa nu sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kusisimua uchumi kupitia seta hiyo muhimu nchini.
Wakizungumza
wakati wa ziara ya Utalii ya
maafisa Tarafa na Watendaji kutoka wilaya ya Iringa iliyoratibiwa na mkuu wa
Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo, walisema kuwa wamefurahishwa na namna
hifadhi hiyo ilivyokuwa na vivutio vingi ambavyo vipi ndani ya hifadhi hiyo.
Emmanuel Ngabuji ni kaimu Afisa Tarafa Pawaga
alisema kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha imejaliwa kuwa na vivutio vingi ambavyo
mtalii akifika katika hifadhi hiyo atafurahia na hatatamani kuongoka kutoka
kuwapata furaha awepo kwenye hifadhi hiyo.
Ngabuji alisema kuwa watendaji wengi imekuwa
mara yao ya kwanza kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha hivyo asilimia kubwa
wamejipanga kwenda kutoa elimu ya utalii kwa wananchi wanaowaongoza huko
katani.
Alisema kuwa amejipanga kuhakikisha wananchi wa
tarafa ya Pawaga wanaandaa Safari maalumu ya kwenda kutembelea hifadhi ya Taifa
Ruaha ili waweze watoto na wananchi wengine kuupenda utalii wa ndani.
Ngabuji alisema kuwa wanamshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo
amekuwa akiutangaza utalii wa ndani kupitia filamu ya Royal Tour ambayo imeanza
kuleta matokeo chanya ya ongezeko la watalii nchi na watalii wa ndani
kuongezeka kutembelea vivutio mbalimbali.
Stella makali na Aunt Mbilinyi ni watendaji wa
kata walisema kuwa wamefurahi kufanya utalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha
baada ya kuona namna ambavyo mnyama Simba anavyofanya mapenzi jambo ambalo
hawajawahi kuliona toka wanzaliwe hivyo inawafanya watafute muda mwingine wa
kwenda kufanya utalii katika hifadhi hiyo.
Walisema kuwa wamefurahia kutembelea hifadhi
hiyo kwa namna ambavyo wameona wanyama mbalimbali na wanavutia kiasi kwamba
ukiwa katika hifadhi hiyo utakuwa na furaha muda wote kwa namna ambavyo vivutio
vingi vilivyopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
"Tumerithishwa,Tuwarithishe tuungane kwa
pamoja kuokomeza ujangili katika hifadhi yetu ya Ruaha iliyopo mkoa wa Iringa
ili hata watoe watu waje waone wanyama na vivutio vilivyomo
hifadhini"alisema makali
Walisema kuwa wanamshukuru mkuu wa wilaya ya
Iringa Mohamed Hassan Moyo kwa kuwaandalia Safari ya kwenda kutembelea hifadhi
ya Taifa ya Ruaha kwa watendaji wa kata na maafisa Tarafa jambo ambalo
limefanyika kwa mara ya kwanza na limekuwa kivutio kikubwa cha kuendelea
kuvitangaza vivutio vilivyopo katika wilaya ya Iringa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa lengo la kuwapeleka maafisa Tarafa na
watendaji kutalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kutambua umuhimu wa
utalii na namna ambavyo wanaweza kuwalinda wanyama pori wasitoweke ili
kuwaliaisha wananchi wengine.
Moyo alisema kuwa maafisa Tarafa na Watendaji
wa Kata kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha kunaongeza chachu ya ongezeko la
watalii katika ukanda wa nyanda za juu kusini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono
jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kusisimua uchumi kupitia seta hiyo
muhimu nchini.
Alisema kuwa viongozi wa serikali za vijiji
kata na Tarafa wanauwezo mkubwa wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhumu wa
kufanya utalii wa ndani na ukaleta tija kwa taifa na wilya ya Iringa kwa ujumla
wake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.