KAMPUNI ya
ununuzi wa Pamba ya Birchand Group ya jijini Mwanza, imeendelea na zoezi la
kuwalipa wakulima wa zao la Pamba katika wilaya zote zinazolima pamba mkoani
hapa.
Kampuni hiyo
imekuwa na utaratibu wa kuwalipa wakulima wa pamba kupitia vyama vya ushirika
vya Msingi AMCOS, kwa kila wiki mara mbili (Jumanne na Jumamosi).
Birchard
group inaendelea kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais DK. John Pombe Magufuli
alilolitoa hivi karibu la kuzitaka kampuni za ununuzi wa pamba kuwalipa
wakulima ndani ya siku 14.
Kauli ya
Rais Dk. Magufuli imekuja ikiwa tayari kampuni hiyo imeishaanza kuwalipa
wakulima wa zao hilo kwa wiki mara mbili ambapo mpaka sasa zoezi hilo
linaendelea.
Baadhi ya
wakulima walionufaika na ulipwaji wa fedha hizo, waliipongeza kampuni hiyo kwa
kuwalipa wakulima kwani kampuni nyingine zilishindwa kununua pamba yao.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Ushirika Cha Msingi (AMCOS) cha Shishani wilayani Magu, Paulo Nzinza
alisema kampuni hiyo imewasaidia kwa
kiasi kikubwa na kuomba serikali kuendelea kuisaidia kwa kuikopesha fedha kama
inavyoendelea kufanya hivi sasa.
Meneja wa
oparesheni wa kampuni hiyo, Steven alisema ndani ya wiki iliyopita wamelipa
wakulima hao kiasi cha Sh. Bilioni 1 na kwamba bado wanaendelea na zoezi hilo
kwa kila wiki kulingana na fedha inavyopatikana.
Alisema
kampuni hiyo pamoja na kuendelea zoezi la kuwalipa wakulima lakini kwa sasa
wana mpango wa kuhakikisha wananunua pamba yote kutoka kwa wakulima wa mkoa
huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.