Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga amewataka wazazi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaita watoto wao majina yasiyoendana na maadili ya kijamii akitolea mfano majina ya wanyama kwa madai kuwa kwa kufanya hivyo ni sawa na kufanya kitendo cha ukatili mtoto husika.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kwenye Viwaja vya Kashaulili mjini Mpanda mkoani Katavi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Juma Homera.
Akizungumzia namna ya kuwajenga watoto kimaadili na kuwatimizia haki zao kama watoto, mkuu huyo wa wilaya amewasisitiza wazazi hao kuwapenda, kuwalinda na kuwajali sambamba na kuwapatia mahitaji muhimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.