Wakulima wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo wa halmashauri ya Wilaya ya Momba katika banda la maonyesho ya nanenane, juu ya njia rahisi ya kupanda mboga za majani kwa kutumia magunia na mifuko hususan mahali pasipo na maeneo ya kupanda bustani.
Mhifadhi wa Mazingira na kilimo hai kutoka Wilaya ya Songwe Noah Ambokile Mbilinyi akitoa maelezo kwa Eddie Mhelela kuhusu aina mpya ya maboga ambayo yana uzito wa Kilogramu 15 mpaka 25 katika banda la wilaya ya Songwe kwenye maonyesho ya nanenane.
Wanafunzi wakijifunza kutoka kwa Afisa Kilimo Sosten Lipamila kuhusu kilimo cha viazi sukari (beetroots) katika banda la halmashauri ya Tunduma, beetroots zina madini mengi ya Calcium hivyo hutumiwa kwa juisi, mboga na chakula na husaidia kuongeza damu.
Mwanzilishi wa kikundi cha kutunza Mazingira cha Estate Vision Amani Zakaria Elias akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza katika banda la maonyesho ya Nanenane katika halmashauri ya Wilaya ya Ileje, kikundi hicho kimeonyesha upekee kwa kuweka miche ya miti ya mtini na mizeituni ambayo ni adimu kupatikana.
Afisa Kilimo kutoka shirika la Norwegian Christian Aid Daniel Isaack akitoa maelezo katika maonyesho ya nanenane kuhusu teknolojia rahisi ya umwagiliaji wa matone ambayo inaweza kutumia maji lita 20 kumwagilia miche 52 ya mbogamboga, wakulima takriban 50 wa wilaya ya Mbozi wameanza kutumia teknolojia hii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.