· Nia ya ziara hii ya siku mbili wilayani Songwe ni kujitambulisha kwa watumishi na taasisi za Wilaya ya Songwe pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo - Brigedia Jenerali Mwangela.
· Nazipongeza taasisi na kampuni mbalimbali ambazo mmeahidi kuendeleza ushirikiano na serikali, wito wangu Wasimame katika ahadi hiyo hiyo hususani ya ushirikiano na serikali katika miradi ya maendeleo inayomgusa mtanzania masikini- Brigedia Jenerali Mwangela.
· Sekta binafsi, watumishi wa umma tunachohitaji ni kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia muda kwakuwa ninaamini bila kufanya hivyo hata kama mna mambo mengi mazuri hamtaweza kufanikiwa- Brigedia Jenerali Mwangela.
· Nasisitiza watumishi tufanye kazi kwa uadilifu, kwa kujituma, kwa weledi na kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na maelekezo mtakayopewa, Nchi yetu inaongozwa kwa sheria na taratibu- Brigedia Jenerali Mwangela.
· Mkandarasi Paulo Philipo Paulo wa kampuni Mats Engineering Ltd anayejenga daraja la Kikamba Wilayani Songwe afanye kazi usiku na mchana ili aweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo Septemba, 2018 kama ilivyo kwenye mkataba, vifaa vya kufanikisha hilo anavyo na mkoa hautakubali pendekezo la kumuongezea muda wa ujenzi - Brigedia Jenerali Mwangela.
· Wilaya ya Songwe ina utajiri mkubwa lakini bila ya kuwa na Amani utajiri huu hautakuwa na maana wala faida kwenu- RPC Songwe Mathias Nyange.
· Kwa kipindi cha Miezi miwili iliyopita Wilaya ya Songwe imeongoza kwa mauaji huku sababu kubwa ikiwa ni Imani za kishirikina, wananchi msiamini Imani hizo zinazopelekea ramli chonganishi maarufu kama lambalamba na kusababisha mauaji hata kati ya ndugu- Brigedia Jenerali Mwangela RPC Songwe Mathias Nyange.
· Ikitokea tena mauaji yaliyosababishwa na ramli chonganishi au Imani nyingine za kishirikina nitahakikisha naanza kumchukulia hatua mtendaji wa kijiji kwa kuruhusu hao watu kufanya shughuli za aina hiyo kijijini kwake- RPC Songwe Mathias Nyange.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.