ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 22, 2018

TUZO YA GAVANA BORA AFRIKA 2018 YANYAKULIWA NA MTANZANIA.


Gavana Mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu, leo May 22, 2018 ametunukiwa tuzo ya Gavana Bora Barani Afrika kwa mwaka 2018 inayotolewa na jarida maarufu la African Banker.

Sherehe za kutoa tuzo hizo, zimefanyika jijini Busan, Korea Kusini, katika mikutano ya mwaka
ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inayoendelea.

“Hii tuzo nimepewa mimi kutokana na mchango mkubwa kutoka BoT wakati wa uongozi wangu. Kwa hiyo, tuzo hii ni heshima kubwa kwangu na kwa Benki Kuu ya Tanzania,” alisema katika mahojiano jijini DSM.

“Awali niliwaomba waandaaji nao walikubali kwamba Dkt. Namajeje Weggoro, Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki apokee tuzo hiyo kwa niaba yangu. Sikujua kama Naibu Gavana wa BoT, Julian Banzi Raphael, anashiriki katika mikutano ya AfDB, vinginevyo yeye ndiye angepokea kwa niaba yangu,” alisema Prof. Ndulu

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa jarida la African Banker, Omar Ben Yedder, Prof. Ndulu ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza huduma jumuishi za kifedha na kuchangia katika kuhakikisha zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanafikiwa na huduma rasmi za kibenki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.