Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto nchini imeahidi kupeleka vitanda katika kituo cha afya cha Lupembe ili kupunguza adha wanazokabiliana nazo wakazi wa eneo hilo pindi wanapokwenda kufuata huduma hususani kwa akina mama wajawazito.
Ahadi hiyo imetolewa na naibu waziri wa wizara hiyo Dkt. Khamis Kigwangalla wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Lupembe muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho na kueleza kuwa serikali ya Rais John Magufuli imedhamiria kuboresha sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya afya. BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI
Kauli ya naibu waziri wa afya imekuja muda mfupi baada ya mbunge wa jimbo hilo Jorum Hongoli kuiomba serikali kusaidia vitanda katika kituo hocho huku akiitaka ijenge hosptali ya wilaya katika eneo hilo ili kupunguza msongamano kwa wagonjwa pindi wanapohitaji huduma za afya.
Wakiongea mbele ya naibu waziri huyo, baadhi ya wananchi wa Lupembe wameiomba serikali kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima vinavyosababishwa na uzembe wa watendaji wake jambo ambalo wamedai kuwa halipaswi kuvumiliwa wala kufumbiwa macho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.