Wadau mbalimbali wamejitokeza kushiriki kwenye sherehe ya uzinduzi nchini Tanzania husussani wale wa jamii ya Shia Ismaili.
Siku hii ina umuhimu mkubwa katika historia ya dhehebu la Shia Ismaili duniani hasa nchini Tanzania kwani ni tukio la kihistoria la kusherehekea kutimia miaka 60 ya uongozi wa Mtukufu MwanaMfalme Karim Aga Khan kama Imamu wa kiukoo wa dhehebu hilo.
Ni sherehe ya maisha ya kazi za Imamu huyo, uthibitisho wake katika uislamu, ambayo inafundisha kuhusu upendo, uvumilivu, amani na heshima kwa binadamu wote. Pia inahusu kujitolea kwake katika kuwaendeleza binadamu wengine.
Katika utamaduni wa kishia, Imamu wao hutumika sio tu kuongoza katika kutekeleza matakwa ya imani lakini pia kuboresha maisha ya wana jamii wanaozunguka mazingira yake na binadamu wengine. Huu ni uongozi unaovuka mipaka ya nchi katika huduma.
Maandamano katikati ya jiji la Mwanza yaliongozwa na Rais wa Baraza la Shia Imami Ismail Magharibi mwa Tanzania Altaf Hirani navyo vyombo mbalimbali vya habari vikichukuwa taarifa ya tukio.
Msafara ukipita katika kipita shoto cha mnara wa Nyerere jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza.
Bango la uhamasishaji wa shughuli za kimaendeleo kuanzia uwezeshaji wa sekta ya elimu, afya, majukumu na tabia.
Ilii kuwa kielelezo kwa kizazi kijacho ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kujua wapi tulipotoka, tulipo na tunakoelekea, Watoto nao wameshiriki maadhimisho.
Na Zephania Mandia – Tarehe 10.7.2017 –
Taasisi za kidini nchini zimetakiwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika uwekezaji wa sekta ya viwanda, ili iweze kutimiza azma yake ya kuwa Taifa lenye viwanda ifikapo mwaka 2025 na hatimaye kufikia uchumi wa kati kupitia sekta hiyo.
Akizungumzia suala hilo Jijini Mwanza, wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya uongozi wa mtukufu Karim Agha Khan, Rais wa dhehebu la Shia Ismail Muslims Kanda ya Ziwa Altafu Hiran Mansoor, amesema dhehebu hilo limeahidi kushirikiana na Serikali katika kuwekeza.
Katika maadhimisho hayo yaliyotanguliwa na maandamano ya kutambua shughuli mbalimbali za kijamii zilizotekelezwa na mtukufu wa dhehebu hilo Aga Khan, amesema hadi sasa dhehebu hilo limeiunga mkono Serikali katika miradi mingi ya maendeleo hasa katika sekta ya elimu.
Kupitia ahadi hiyo katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Clodwin Mtweve, aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela katika tukio hilo, ameushauri uongozi wa shule zinazomilikiwa na dhehehebu hilo kuzalisha wataalamu wengi wa fani ya Sayansi.
Awali akizungumzia umuhimu wa maadhimisho ya miaka 60 ya uongozi wa mtukufu Karim Aga Khan, Rais wa dhehebu hilo Kanda ya Ziwa Altaf Hiran Mansoor, amesema ni tukio la kihistoria kwa waumini kwa kuwa linang’aza uthibitisho wa imani yake.
Wazo la kuisaidia jamii na kuleta matumaini miongoni mwa jamii, ni la kihistoria katika jamii ya kiislamu ya Shia Ismail, ambalo limekuwepo kwa miaka 1,400 iliyopita, wakati wa nyakati za mwanzo za Uislamu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.