ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 10, 2017

LUKAKU SASA RASMI MANCHESTER UNITED.

KLABU ya Manchester United imefanya usajili wa pili dirisha hili, baada ya kumnasa mshambuliaji hatari, Romelu Lukaku anayevunja rekodi ya dau kubwa la usajili.
Kukamilika kwa dili hilo inamaanisha kocha Mreno, Jose Mourinho ameipiku klabu yake ya zamani, Chelsea katika vita ya kuwania saini ya Mbelgiji huyo.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anahamia Old Trafford kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 75 - inayomfanya awe mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka ya Uingereza.


Lukaku amesaini mkataba wa miaka mitano wenye kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja zaidi.


"Ningependa kuanza kuwashukuru Everton na mashabiki kwa misimu minne ya aina yake iliyopita, nimetengeneza marafiki fulani maalum na tumekuwa na wakati fulani mzuri pamoja," amesema Lukaku na kununukuliwa na tovuti ya United.



"Pamoja na hayo, wakati Manchester United na Jose Mourinho wanakuja kugonga mlango ni fursa nzuri maishani ambayo nisingeweza kukataa," amesema.

"Unaweza kuona mpambano, kujituma na morali katika timu hii wakati wa fainali ya Europa League nami ninataka kuwa sehemu ya hii. Siwezi kuacha kwenda kukimbia Old Trafford mbele ya mashabiki 75,000, lakini kabla ya kujinadaa na msimu, ndiko ambako kujituma kunaanzia na ninaangalia mbele kuelekea awamu ya kwanza mazoezi,"amesema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.