Siku ya tukio mwanaume huyo akiwa nyumbani alipokea simu kutoka kwa mwanakijiji wa kike , wanayefahamiana, na ambaye alikuwa akitumia simu ya mkewe, na kudai ilikuwa imeokotwa barabarani na watoto. Pia alimtaka amueleze mkewe aende akaichukue kwake.
Lakini alipomaliza kuongea kwa simu, mkewe ambaye alikuwa pembeni yake alimshutumu kuwa alikuwa akimsengenya kwa simu na mwanamke mwingine na kutaka kujua kwa nini alikuwa akifanya hivyo.
Bw Kamau ambaye hufanya vibarua ili kujikimu alijaribu kueleza kilichotokea bila mafanikio. “Vita vilianza na nilifaulu kumwangusha chini. Niliwacha kumpiga na kisha kumuonya dhidi ya kuibua shtuma zisizokuwa na msingi, na kutumia nafasi hiyo kumuelezea nilichokuwa nikiongea kwa simu,” alisema.
Lakini akiwa anaendelea na mazungumzo na mkewe akiwa chini, mwanae wa kiume alichukua upanga na kumgonga nao nyuma ya kichwa, na kumfanya apoteze fahamu. Hata hivyo, alidai kuwa mkewe alichukua panga kutoka kwa mwanae na kumkata sehemu nyeti kabla ya kutoroka. “Nilipopata fahamu nilihisi maumivu makali na kugundua nilikuwa nikivuja damu kichwani na katika sehemu nyeti, kabla ya kugundua walikuwa wamenikata na kuniumiza vibaya,” alisema akiongeza kuwa alipotazama alimuona mkewe na mwanae wakitoroka.
Hata hivyo, alifanikiwa kupiga kelele za msaada zilizovuta majirani ambao pia walimkamata mkewe, na pia kumpeleka Bw Kamau kwenye kliniki ya Kanisa la Presbyterian Church of East Africa Uplands kabla ya kuhamishwa hospitali ya Kijabe.
Kaimu afisa mkuu wa polisi, Bw Stanley Mutungi amesema wanamzuilia mama huyo wakati uchunguzi ukiendelea.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.