Mmiliki wa Kiwanda cha Chobo Investment, Bw. John Chobo
(mbele) akiwaongoza viongozi wa Benki ya Kilimo
kutembelea kiwanda hicho. Aliofutana nao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo
wa TADB, Bw. Augustino Matutu
Chacha (kushoto).
Ugeni kutoka TADB ukijionea nyama iliyohifadhiwa kwenye jokofu (chiller) kusubiri kuchakatwa kabla kupelekwa sokoni.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo,
Bw. Charles Hotar akionesha mashine ya kuchakatia nyama kwa ajili ya
kutengenezea soseji kwa wageni kutoka Benki ya Kilimo
(hawapo pichani).
Mtaalamu kutoka Idara ya Soseji wa wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Stanley Kirio akiendelea na zoezi la kuandaa soseji.
Meneja
Uendeshaji wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Charles Hotar (kushoto) akionesha
soseji zilizokuwa katika hatua za ufungaji. Wanaomuangalia ni wageni
kutoka Benki
ya Kilimo.
Mmiliki wa Kiwanda cha Chobo Investment, Bw. John Chobo
(kulia) akiwaonesha vifungashio vya soseji zilizotayari kupelekwa sokoni. Wanaomtazama ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga (kushoto) na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw.
Augustino Matutu Chacha (katikati).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akionja soseji za Kiwanda cha Chobo.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Chobo wakichapa kazi.
TADB
yavutiwa na Kiwanda cha Chobo
Na mwandishi wetu, Mwanza
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema imeridhishwa na uwekezaji wa Kiwanda
cha Nyama cha Chobo kilichombo Misungwi jijini Mwanza kwa kuwa kinawahakikishia wakulima wadogo masoko ya mifugo yao.
Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati alipofanya
ziara ya kujionea maendeleo ya uwekezaji wa miundombinu ya Kiwanda hicho.
Bw. Assenga amesema kuwa Kiwanda cha Chobo ambayo inamilikiwa na kijana mzalendo, John Chobo
ina uwezo mkubwa wa kusadia wakulima wadogo kwa kununua mifugo yako hivyo kuwapatia fursa za
masoko wakulima hao.
“Miundombinu ya Kiwanda inaweza kuchinja zaidi ya ng’ombe 600 kwa siku, hili ni soko kubwa
sana kwa wakulima wadogo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hali itakayounga mkono juhudi za serikali hasa TADB katika kuboresha
minyororo ya thamani kwenye sekta ya mifugo,” alisema.
Bw.
Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB)
ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili
kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza
mapinduzi katika
kilimo nchini.
Bw.
Assenga ameongeza kuwa sekta ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya
mwanzo inayopatiwa
mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali
hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na
maziwa nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe
wa Nyama na Maziwa.
“Benki
inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa
mitambo na ufungaji
wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya
kunyweshea na pamoja na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya
kuongeza thamani nyama na maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Mmiliki wa Kiwanda hicho, Bw. John Chobo alisema
kuwa kwa
sasa kiwanda chake hakijafikia uwezo wa kutumika kwa asilimia 100
kutokana na changamoto za kimtaji zinazomkabili na alitumia fursa hiyo
kuiomba Benki ya Kilimo kumuwezesha ili aweze kutoa ajira zaidi kwa
Watanzania.
Kwa mujibu wa Bw. Chobo kwa sasa kiwanda chake kina wafanyakazi 85 na kikifikia uwezo wa kuzalisha
kwa asilimia 100 kitaweza kuajiri zaidi ya wafanyakazi 300 watakaofanya kazi kiwandani na 300 watakaokuwa wakisimamia shamba.
“Tunaiomba
TADB kutatulia changamoto za ukosefu wa mitaji ya uhakika kwa kuwa kwa
kiasi kikubwa
na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande
wa biashara za bidhaa na ambayo riba yake ni kubwa sana.,” alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.