ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 18, 2017

MIILI YA WANAJESHI WA SERIKALI YAPATIKANA KASKAZINI MWA MALI.

Duru za usalama za Mali zimetangaza habari ya kupatikana miili ya wanajeshi wanane wa serikali, kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Shirika la habari la Reuters limezinukuu duru za usalama za Mali zikitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, wanajeshi hao wanane wameuliwa wiki iliyopita katika shambulizo la watu wenye silaha katika maeneo ya Gao na Menaka, kaskazini mwa Mali.
Mwezi Machi 2012, maeneo ya kaskazini mwa Mali yalitekwa na makundi yenye misimamo mikali ambayo yana uhusiano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida.
 Operesheni ya kupambana na mgaidi nchini Mali
Mwezi Januari 2013, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa walitumwa nchini Mali chini ya mwavuli wa kikosi cha MINUSMA kwa ajili ya kupambana na makundi yenye misimamo mikali.
Hata hivyo hadi leo hii askari hao na wale wa serikali wameshindwa kukomboa maeneo kadhaa ya kaskazini mwa Mali.
Makundi hayo ya kigaidi yamekuwa yakifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya maafisa usalama wa serikali, askari wa kigeni wanaolinda amani nchini Mali pamoja na raia wa nchi hiyo.
Habari ya kupatikana miili hiyo ya wanajeshi wa Mali imekuja siku chache baada ya jeshi la nchi hiyo kutangaza kuwa, limemuangamiza mkuu wa kundi lenye misimamo ya kufurutu ada katikati mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo lilitangaza kuwa, limefanikiwa kumuua Bekaye SangarĂ©, kiongozi wa kundi lenye misimamo mikali ya kigaidi linalojiita 'Harakati ya Ukombozi wa Macina' katika kijiji cha Mougna karibu na mji wa Mopti wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.