Na: Edwin Soko
Jahannesburg
Afrika ya Kusini
Mkutano wa kimataifa wa bara la Afrika juu ya uandishi wa habari za uchunguzi umeanza leo Mjini Jahannesburg Afrika ya kusini kwa Waandishi wa habari toka Nchi mbalimbali kushiriki wakiwemo wanaotoka Nchini Tanzania.
Mkutano huo wa siku tatu kuanzia Novemba 7hadi 9, 2016 unafanyika kwenye Chuo Kikuu cha Wits kilichopo Jahannesburg huku malengo makuu yakiwa ni kuwaleta Waandishi pamoja ili washiriki kwenye kujadili matatizo ya kitaaluma yanayoikabili tasnia ya habari Afrika hasa wakati wa kuripoti habari za uchunguzi.
Akiongea na Waandishi wa habari wanaoiwakilisha Tanzania kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania, Bw. Earnest Sungura amesema kuwa, mkutano huo untawapa fursa washiriki toka Tanzania kujifunza changamoto za uandishi wa kiuchunguzi toka kwa washiriki wa Nchi mbalimbali na kubadilishana uzoefu.
“Lengo la kuwachagua miongoni mwenu ili mhudhurie mkutano huu ni kutaka kuongeza thamani za kazi zenu mnazozifanya kwenye miradi mliyoomba ili ziweze kuwa na thamani kubwa kwa kulinganisha na masuala yatakayojadiliwa kwenye mkutano huu”, Alisema Sungura
Kwenye mkutano huo mada mbalimbali zitawakilishwa ikiwemo usalama wa Mwandishi na vifaa vyake, kuripoti habari za kitakwimu, migogoro inayochochewa na rasilimali za Afrika, pia kutakuwa na mada zitakazowasilishwa na mabingwa wa habari za uchokonozi kama Mohammed Ally , Mwandishi anayetoka kituo cha luninga cha KTN.
Tanzania imewakilishwa na Waandishi wanne chini ya ufadhili wa TMF, ambao ni Veronika Mataba (Radio Faraja), Edwin Soko (Redio SAUT FM), Irene Mbakilwa(TBC Iringa), na Nicholas Ngaiza(Radio Kasibante Kagera)
Chi ishirini na mbili zinahudhuria mkutano huo.
Wakiongea kwa pamoja wameahidi kujifunza mengi yatakayoweza kuisaidia Tasnia ya habari Tanzania ili kuchangia kwenye kukuza maendeleo ya Nchi kwa kuzingatia msingi mkubwa wa ukweli kwenye uandishi wa habari.
Wakati huo Waandishi wa Kenya wameutaja muswada wa sheria ya vyombo vya habari ulipitishwa na bunge hivi karibunu kuwa ni muswada mbaya sana ambao unadhoofisha taasnia ya habari Tanzania.
“Nimusoma muswada huo naona ni mbaya kuliko katika ukanda wa Nchi za Afrika ya mashariki, pia nahisi kwa sasa kuna ajenda ya Afrika ya Mashariki kuviminya vyombo vya habari” Alisema Mwandshi John Allan toka standard Group ya Kenya”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.