NGUMI ZA KULIPWA KIZUNGUMKUTI
Hivi karibuni kumetokea na migongano ya kisheria na fitna ndani ya ngumi za kulipwa na baadhi ya wavamizi kuitumia nafasi hiyo kuisambaratisha kama sio kuua kabisa tasnia ya ngumi za kulipwa.kwa kujaribu kufanya mapinduzi.
Ukweli ni kuwa kwa muda mrefu sana ngumi za kulipwa hapa nchini zilikuwa zikiendeshwa na kuongozwa na makampuni hasa PST na TPBO huku TPBC nayo ikijikokota kwa nyuma yao likisimamia jina bila kuwa na mapambano mengi ya kueleweka. Huku mapambano yote makubwa na maubingwa yakisimamiwa na makampuni hayo na mawaziri wenye dhamana husika wakiwa ndio wageni rasmi na kutoa michango yao, kwa TPBO au PST au TPBC ltd, sasa iweje leo hawakubaliki?
Tukumbuke TPBC ilikuja baada ya migogoro ya BUT ambao ni chama waanzilishi wa ngumi za kulipwa ndio maana nikasema likisimamia jina lisipotee kwa kuwa hawakuwa wakifanya kazi zozote kwa mda mrefu.
Baada ya kuzaliwa tpbc hakukuwa na maendeleo mazuri kupelekea migogoro isiyokwisha na kuzaliwa makampuni binafsi ya PST ,TPBO na mengineyo ambayo ndio yaliyofufua tena ngumi za kulipwa na kuanza kupata umaarufu na mabingwa tofauti na mabondia kupata mapambano mengi ya nje ambayo yamewafanya mabondia wengi kujiajiri na kupata kipato cha kuwakwamua kupitia mchezo huu wa ngumi. Ushindani nao wa mabondia ukaanza ongezeka ,ma gym ya ngumi yanaongezeka nayo pia yakawa na ushindani na kuhakikisha wanajitahidi kutoa mabondia wengi wazuri zaidi.
Mabondia wakiwa wanaamini mapambano ya kimataifa ndio yana malipo mazuri kulinganisha na mapambano ya kawaida ya ndani ya nchi hivyo kila bondia wa kulipwa alijitahidi acheze mapambano mengi zaidi hata kwa gharama ndogo ili awe na rekodi itakayomwezesha kupata mapambano yenye kiwango kizuri cha pesa .
Ngumi zikawa zinapigwa viwango vinaongezeka kila bondia na mdau wa ngumi wakirudisha imani kwa mchezo wa ngumi za kulipwa na mategemeo makubwa zaidi kwa kiwango cha hali ya juu.mambo yakawa yanakwenda raha mustarehe kuelekea kilele cha ubora duniani.
Kwa nia njema ya kuendeleza huu mchezo usonge mbele na ufike hapo kileleni , makampuni yote kwa pamoja yakaonelea yaanzishe umoja wao kwa ajili ya kupeana utaalamu na kuwa na msemaji pindi itakapohitajika kuelezea muenendo wa ngumi,huku kila kampuni ikiendelea na shughuli zake kama kawaida za ngumi ,
washirikiane kwa pamoja kutanua wigo wa ushindi na mafanikio ya ndani na nje ya Tanzania,
Wakaonelea katika umoja huo washirikishe mdau wa michezo toka serikalini maana nguvu nyingi ishatumika kibinafsi na kwa kuupa heshima zaidi mchezo wa ngumi za kulipwa , hapo wakapendekeza ,wawashirikishe baraza la michezo liwe karibu na ngumi za kulipwa kwa lengo la kusaidiana kutatua matatizo na utaalamu.
wakitambua baraza la michezo linajishuhulisha zaidi na ngumi za ridhaa.
na miaka ya hivi karibuni ngumi za ridhaa zimekuwa haziendi vizuri zimedorola na kushindwa kufuzu kufanya vizuri katika mashindano mengi ,na ngumi za ridhaa zipo chini ya baraza la michezo kupitia shirikisho lao la BFT ,
hivyo baraza lilitakiwa kuongeza umakini na BFT kuhakikisha wanafanya vizuri , mabondia medali zinapatikana ,mabondia wanafuzu kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola , olyimpics na mashindano yote makubwa yanayohusiana na ngumi za ridhaa, mikakati ya BMT bado haijaeleweka kuinusuru ngumi za ridhaa.
na msingi mzuri wa ngumi za ridhaa(amacha) ndio unaoleta na kuzaa mabondia wazuri sana wa ngumi kulipwa(professional boxers). Kukiwa na mabondia wengi walioshiriki olyimpic na kadhalika ,wakijiunga na ngumi za kulipwa tayari washakuwa mabondia wazuri na ni rahisi kufundishwa kwa ajili ya maandalizi ya ubingwa hapo ni kazi ya makampuni na mashirikisho ya kulipwa kumuendeleza katika ajira yake hiyo (professional boxing) na kutuletea mataji.
Baraza la michezo Tanzania(BMT) kupitia kaimu katibu wake bw Mohamed kiganja wakakubaliana na hilo la makampuni yote kuwa na bodi na akawapa mamlaka ya kujichagua viongozi wa muda na kutunga katiba ambayo ndiyo itakayoendesha haya makampuni yote ya ngumi za kulipwa hapa nchini.
Akachaguliwa bw habibu kinyogoli (KBF) kama mwenyekiti. Emmanuel mlundwa (PST) katibu mkuu na chaulembo palasa(TPBC) kama katibu msaidizi, Yasin Abdallah (TPBO) na Onesmo ngowi(TPBC ltd) kama wajumbe.
“hapa ukiangalia mashirikisho yote makubwa ya ngumi za kulipwa Tanzania yamehusika “.MUENENDO HURU USIO NA UPENDELEO WOWOTE.
Wakajichagua na kupendekeza jina la TANZANIA BOXING AUTHORITY (TBA) .
Na katiba itengenezwe mara moja watu wapige kazi.
wakiwa katika kipindi cha mchakato wa utengenezaji wa katiba kampuni ya PST ikawa na skendo la uendeshaji wa mchezo na kupelekea TPBC na TPBO kuchochea kufungiwa huku, TPBC ltd ikitulia, TPBC na TPBO wakajichagua tena uongozi mpya kutengeneza katiba ya TBA bila kuwashirikisha makampuni mengine.huku msimamizi wa zoezi hilo bw kiganja kutolifuatilia.
Wakati PST ikiwa katika mchakato wa rufaa na kupinga adhabu iliyopewa, katika hali isiyo ya kawaida kaimu katibu mkuu bmt Mohamed kiganja akateua kwa maneno TPBC kuwa ndie msimamizi mkuu wa ngumi za kulipwa nchini bila kuwashirikisha makampuni mengine. Huku akisahau kuwa hapo awali TPBC,TPBC LTD,PST,TPBO na makampuni mengine yote yalikuwa yakifanya kazi zao sawa na muelekeo wa kufika kileleni(mafanikio)
,huku hao tpbc wakiwa hawana nguvu sana wala wataalamu wa kutosha wa ngumi kulinganisha na makampuni mengine. Wala uwezo wa kusimamamia mapambano makubwa ya ubingwa.
TPBC walianza kulitumia vizuri rungu hilo walilopewa na BMT kwa kuhakikisha mapambano yote yaliyo chini ya PST au TPBO yanaharibika au wanasimamia wao .,jambo lililopelekea mapambano mengi kuvunjika na mapambano waliolazimisha yakichezwa kwa chini ya kiwango na nje ya malengo,
kwa mfano tumeona likifanyika pambano kubwa la mamilion ambalo lilikuwa lisimamiwe kwa ushirika wa tpbo na pst ambao wangewakilisha mikanda ya UBO na WBF ambayo dula mbabe alicheza na mchina, na ibrahim class alikuwa acheze na bondia kutoka south afrika halikufanyika baada yake south kukataa kucheza pambano lisilo la ubingwa na kubadilishiwa mpinzani kiholela,
juu ya kutumika mamilion kuandaa na udhamini ikashindikana kuchezwa ubingwa,na mapambano kadhaa wa kadhaa madogo yakishindwa kuendeshwa ipasavyo, huku mapromota wakiingia hasara na kuwa na manunguniko ya hapa na pale wakilalamika ngumi zinapokwendea.
Jambo lililoleta sintonfahamu katika tasnia ya ngumi za kulipwa ni pale TPBC kulazimisha makampuni mengine ya ngumi na wadau wote wachukue vibali vya ngumi kwao wao wakiwa kama ndio wakala wa serikali na wasimamizi wa ngumi za kulipwa Tanzania kwa mamlaka waliyopeana na BMT kwa vigezo wanavyojua wenyewe pindi kuna manunguniko ya rushwa na urafiki kuingizwa katika uteuzi huo. Kwa hiyo hapa inaonekana kosa kubwa ni wadau wa ngumi za kulipwa kujihusisha na bmt ambao ngumi zinazowahusu kwa asilimia mia ni za ridhaa zinawashinda kuziendesha kila leo mabondia wana hali ngumu sasa iweje leo wameshirikishwa kuuinua mchezo wa ngumi , wao wanageuza kitega uchumi na kuingiza urafiki/undugu kupiga dili kupitia ngumi za kulipwa.
Hivi sasa kumekuwa na maskendo ya hapa na pale katika tasnia ya ngumi za kulipwa huku Tpbc wakizuia mabondia mapambano yao na kudiriki kuharibu hata safari za nje za mabondia .misukosuko hii imepelekea kama bondia ukiwa karibu na kiongozi wa kampuni Fulani ukicheza pambano hutopewa ushindi iwapo umeshinda . ni mambo yanayoongeza chuki na uhasama kati ya viongozi wenyewe na mabondia pia kutokuwa na imani na mchezo wa ngumi.
Tpbc wakidai wao ni wakala wa serikali kupitia BMT ,wamekuwa ni kero kwenye mzunguko mzima wa ngumi za kulipwa kwa kukusanya pesa ambazo hazijulikani zinakwenda wapi . wamekuwa wakikusanya pesa za matamasha ,vibali vya mapambano leseni nk. TPBC hailipi kodi ikidai yenyewe ni bodi huku inaandaa mapambano yake na kusimamia maubingwa yake yenyewe ,ikizuia wengine wasifanye kazi hizo kama si watu wao.
Wadau wa mchezo wa ngumi kikubwa wanachojiuliza na wasiwasi wao kwa hao wahusika waliopo huko tpbc wamepewaje mamlaka hayo makubwa bila kuhusishwa wadau wakuu wa mchezo wenyewe,pia hao viongozi waliokuwepo wameshawahi kutuhumiwa kujihusisha na biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya na ofisi wamepewa ndani ya majengo ya serikali.pia wengine walishajaribu kuuteka mchezo wa pooltable kwa njia kama hizihizi walizotekea ngumi, kwanini huku kwenye ngumi wapewe majukumu wasiyoyajua kiutaalam wa mchezo wawe wanahusika na safari za nje na ukusanyaji wapesa tu.tunajiuliza hapa kuna namna!!?
Mapendekezo ya wanamasumbwi walio wengi katika kuunusuru mchezo wa ngumi hapa ulipo ni kuwa waitwe wadau wakuu na makampuni yote yanayojihusisha na ngumi za kulipwa mbele ya waziri mwenye dhamana husika akisimamia umaliziaji wa utengenezaji wa katiba ya TANZANIA BOXING AUTHORITY (TBA), ambayo itawajumuisha viongozi wote na wataalam wote wangumi za kulipwa hiyo TBA ndio itakayokuwa ikisimamia uendeshaji wa ngumi za kulipwa, UFANYIKE UCHAGUZI MWINGINE HURU WATAKAOSIMAMIA HIYO TANZANIA BOXING AUTHORIY (bodi)
Sio kama ilivyo kwa sasa tpbc inajiita chama wakati haina uchaguzi,na ndio waliojitwika madaraka kupitia katibu mkuu BMT wakati wao ni kikundi kidogo cha wajanja Fulani kinachofadhiliwa na mwanasiasa mkongwe anayewania madaraka makubwa serikalini ,sasa tumekuwa wanamichezo ni watu wa wakutumiwa kibiashara chafu za madili na siasa.ofisi za TPBC zimehamia ndani ya ofisi za BMT tukiwa kama wadau wa ngumi hatuelewi zinalipiwaje au kwa ufadhili gani?
Waziri mwenye dhamana husika . okoa hili kabla halijaoza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.