Katika kusheherekea siku ya mtoto wa kike kimataifa, ninawaletea kisa kifupi chenye mafunzo muhimu kwa wasichana wote duniani, kisa hichi ni cha MAYA.
Maya ni binti wa miaka 12 aishie na wadogo zake wawili wa kiume katika familia maskini. “Ndoto” yake ni kuwa mwalimu ili kuisaidia jamii yake. Umasikini wa familia yake wamfanya Maya kukaa nyumbani na wadogo zake kwenda shule. Ndoto yake imevunjika. Maya hana elimu wala ajira (takwimu zaonyesha 1/3 ya wanawake Tanzania hawajasoma).
Maya anajihatarisha kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI (huku asilimia 40 tu ya wasichana umri kati ya 15-19 wakiwa na elimu juu ya ugonjwa huu) au mimba ya utotoni kwa kujiuza ilia apate chakula, hifadhi na ulinzi. Anapata uja uzito akiwa na miaka 16 (huku ¼ ya wasichana kuaniza umri wa miaka 15 ni wazazi watoto).
Anajifungua kwa matatizo mtoto Maryam ambapo anaamua kubadili msimamo wa maisha yake.
Anajifungua kwa matatizo mtoto Maryam ambapo anaamua kubadili msimamo wa maisha yake.
Maya anajihusisha na kazi za kuajiriwa na biashara ndogo, anafanikiwa kufungua mgahawa. Sasa anaweza kumpeleka Maryam shule.
Maryam anasoma kwa bidii na kupata udhamini wa kwenda chuo ambapo anafanikiwa kuhitimu kama Mwalimu. Mustakabali wake sasa uko mikononi mwake tofauti na ule wa Maya, na sasa Maryam anaweza kusaidia jamii yake, ndoto ambayo alikuwa nayo mama yake.
Kumbuka: Ukimuelimisha mwanaume unamueleimisha mtu mmoja, ukimuelimisha mwanamke basi unalielimisha Taifa!
Tazama video hii fupi hapa chini upate kuelimika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.