Ndege hizo aina ya Bombardier Q400 zilizotengenezwa na kiwanda cha Bombardier nchini Canada zinatarajiwa kuzinduliwa kesho kuanzia majira ya saa 2.00 asubuhi katika uwanja wa JNIA (Terminal 1).
Katibu Mkuu wa (Uchukuzi) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk. Leonard Chamuriho amesema Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ndege hizo.
Aidha, ndege ya kwanza iliwasili Septemba 20,2016. Ndege hizo zina uwezo wa kubeba abiria 76 kwa kila moja ambazo zitahudumia soko la ndani na nchi jirani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.