ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 27, 2016

ZOLA TANZANIA YAZIONDOA GIZANI SHULE 7 MWANZA.


MWANZA
KAMPUNI ya Zola Tanzania imezifunga  bure mitambo ya  umeme wa sola ya jua katika shule saba za serikali na binafsi ndani ya  Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuondokana na adha ya kukosa mwanga wa uhakika pamoja na athari zitokanazo na hitilafu za umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo muda mfupi baada ya ufunguzi wa duka la kuuza mitambo yao,Meneja Masoko wa kampuni hiyo Mkoa wa Mwanza, Emmenuel Meisila alisema  lengo  kubwa  ni kurahisisha  maisha na kuwezesha wananchi kupata mwanga wa nyumbani na biashara.

Meisila alisema licha ya mitambo huyo kuuzwa kwa wananchi kwa gharama nafuu lakini wameamua kuzifungia shule za Serikali na binafsi bila malipo ili wananfunzi waweze kupata mwanga na kujisomea nyakati za usiku.

 Alizitaja shule zilizofungiwa mitambo hiyo ni Sekondari ya Nundu, Kabuhoro, Kangaye, Eden Valley, Glory ambapo shule za msingi ni Bezi na Rishor.Aliongeza kuwa shule zingine  227 zimefungiwa mitambo katika mikoa tofauti hapa nchini.

“Kila mtambo  mmoja tuliofunga katika  shule umegharimu Sh milioni 1.2, sasa ukijumlisha gharama zote utabaini ni zaidi ya Sh milioni 9 tumeamia kufanya hivyo kwa nia njema ya kuisadia Serikali na watu binafsi kupata mwanga katika shule zao, bado tunaendelea kutoa misaada mingine ya kijamii.

“Awali tulikuwa tunajulikana kama M Power lakini kukawa na mwingiliano na kampuni zingine tukaona tubadili jina, kumekuwapo na propaganda kwmaba tunaelekea kufilisika huku wengine wakidai tunakwepa kodi, yote hayo ni uongo.
“Tunawaahidi wateja wetu tutaendelea kufanya maboresha na hivi karibuni tutakuja na sola zenye uwezo wa kuwasha jokofu na mitambo mingine mikubwa, mpaka sasa hapa Mwanza tunao wateja 15,000 lakini lengo letu kwa mwaka huu ni kuwafikia 25,000,”alisema.
Meisila alisema umeme wa sola  ndio unapaswa kufungwa kwenye mabweni ya wanafunzi ili kuepuka athari zinajitokeza kwa sasa ikiwamo kuungua moto na kusababisha hasara kwa Serikali.

Alisema matumizi umeme wa Tanesco kwa  wanafunzi wa bweni ni hatari kwani wengi hutumia bila kuchukua tahadhari lakini kwa upande wa sola hakuna madhara yoyote.

Pia alisema licha ya Serikali kujitahidi kusambaza umeme kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini(REA) bado Zola Tanzania ina nafasi kubwa ya kupata wateja kutokana na gharama nafuu pamoja na ofa wanayopata ya redio na televisheni.

Naye Meneja Masoko Kanda ya Ziwa, Mathew Dunia, alisema lengo lao nu kuwafikia wateja milioni moja na kubainisha kwamba wameamua kupunguza miaka ya kumilikishwa mitambo yao kutoka 10 hadi mitatu na kumhudumia mteja kwa kipindi cha miaka mitano bila malipo.

Hata hivyo alisema ili kuwaondoa hofu kwa wateja wao, kampuni imekusudia kufanya marekebisho katika ujumbe unaotumwa wakati wa malipo ili kuonyesha salio halisi la mitambo yao.

Naye Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Nyamagana Magharibi ambaye aliwakilisha viongozi mitaa ya Wilaya ya Nyamagana, Julius Saimon ujio wa kampuni hiyo ni mkombozi wa wananchi wasio na uwezo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.