Uwepo wa wanafunzi hao unaashiria moja kwa moja ulaji fedha zilizotengwa na Rais John Magufuli alizotenga kwa ajili ya kugharimia elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mtaka alisema kutokana na taarifa za awali za kuwepo kwa wanafunzi hewa, ameagiza kuvuliwa vyeo kwa walimu wote wakuu wa shule hizo, lakini pia wanaandaa mpango maalumu wa kuwafanyia uhakiki walimu wote wakuu ili kujua tabia na mienendo yao kabla ya kuwapa wadhifa huo.
Alisema katika uhakiki wa wanafunzi kwa shule za msingi na sekondari mkoa mzima, taarifa za awali zimeonesha mpaka sasa katika shule za sekondari wamebainika kuwepo wanafunzi hewa 2,331 na bado unaendelea na pindi ukikamilika atatoa taarifa kamili.
Alisema kwa upande wa shule za msingi, kazi inaendelea na upande wa shule za sekondari wilaya pekee ambayo haikuwa na wanafunzi hewa ni Bariadi huku wilaya ya Itilima ikiwa na wanafunzi hewa 2,137, Meatu 121, Busega 110 na Maswa imebainika kuwa na wanafunzi hewa 14 na kazi ya uhakiki bado inaendelea.
“Mkoa wa Simiyu una jumla ya shule za msingi za serikali 516 na shule za sekondari 140, ambapo jumla ya walimu wakuu wa shule zote wapatao 656 watavuliwa madaraka yao kuanzia sasa,” alisema Mtaka aliyemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Jumanne Sagini kuwavua madaraka mara moja wakuu wote 140 wa shule za sekondari mkoani humo kutokana na kugundulika uwepo wa wanafunzi hewa.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.