ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 30, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA KIBAHA MJINI ACHANGIA MILIONI 5 UJENZI WA DARAJA LA PANGANI LIKAKALOJENGWA NA JWTZ

Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka wa katikati  akikagua sehemu ambayo itajengwa daraja hilo la pangani, ambalo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 36, ambapo daraja hilo linatarajiwa kujengwa chini ya usimamizi wa JWTZ.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

MBUNGE wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amechangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha daraja litakalounganisha kata ya pangani iliyopo halmashauri ya mji Kibaha Mkoa wa Pwani na mpiji magoe iliyopo kata ya kibamba manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Daraja hilo ambalo linatarajia kujengwa kwa ushirikinao wa  Jeshi la wanachi Tanzania (JWTZ) litakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya Kibaha pamoja na wale wanaotoka katika kata ya kibamba sambaamba na kuwasaidia wanafunzi pamoja na wakinamama  ambao walikuwa wanashindwa kuvuka wakati wa masika.

Akizungumza katika halfa ya fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kufanya harambee wa daraja hilo Koka amesema litagharimu milioni 36 na kwamba  JWTZ  tayari  wameshakubali kusaidia ujenzi huo ambapo ukikamilika utaweza kutoa fursa mbali mbali za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo lake  pamoja na kuondokana na kero ya kuvuka nyakati  za masika.
Mimi kama mbunge wenu hii changamoto ya wananchi wangu naifahamu kwani wamekuwa wakipata tabu sana wakati wa kuvuka hasa katika kipindi cha mvua ukizingatia daraja hii lilolopo kwa sasa linahatarisha masiha ya watu kutokana limejengwa kwa miti,lakini hili ambalo litajengwa na JWTZ litaweza kusaidia na kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa panagani na maneo mengine,”alisema Koka.

Aidha Koka aliongeza kuwa katika kuhakikisha daraja hilo linajengwa ataendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo wawekezaji ambao wamewekeza katika kata ya pangani ili waeze kusaidiana nao na kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea ya kuwaletea mabadiiko chanya ya kimaendeleo.

Kwa upande wao  baadhi ya wananchi  wa kata ya pangani akiwemo Musa Maige pamoja na Hamisi Ugo Wananchi wanapata shida kubwa ya kufuata huduma za afya kwani wanatembea zaidi ya umbali wa kilometa 11 mpaka maili moja  na kupelekea wakati mwingine  baadhi ya wakinamama wajawazito kujifungulia njiani wakati wakwenda kupatiwa matibabu.

Mmoja wa wakinamama aliyejtambuisha kwa jina la Subira Ally  hapa anaelezea jinsi wanavyopata shida hasa  wakati wa kujifungua, pamoja na watoto wao ambao wanasoma shule wanavyopata shida katika kipindi cha masika kwani daraja linajaa maji na kujikuta wanashindwa kuvuka katika  mto huo.  

Nae Diwani wa Kata ya Pangani Augustino Mdachi alisema kwamba kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutaweza kuwasaidia wananchi wake ambao walikuwa wanateseka kwa kipindi cha muda mrefu kuweza kuvuka kwa urahisi na kuendelea kufanya shughuli za mbali mbali za uzalishaji na kuleta maendeleo.

Awali akisoma risala katika hafla hiyo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Pangani Abdlah Ngulengule hapa anabainisha changamoto ambazo zinakwamisha kuanza kwa ujenzi huo wa daraja pamoja na mikakati waliyojiwekea ili kufanikisha zoezi hilo.
 
KIVUKO cha  awali ambacho walikuwa wanakitumia ni cha miti hivyo wakati wa mvua inaponyesha kinafunikwa na maji hivyo kuwapa wakati mgumu wananchi hao na kuwalazimu kutumia usafiri wa pikipiki kwenda maili moja kwa ajili ya kufuata huduma   ambapo nauli ni kati y sh.20000 hadi 30000.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.