ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 27, 2016

UTEUZI MWINGINE WA RAIS MAGUFULI LEO 27JULY 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Bw. Oliva Paul Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Aidha, Rais Magufuli amemuapisha Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC).

Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu July 15 2016, viongozi hao wanakuwa wa kwanza kuongoza Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) tangu Tume hiyo ilipoundwa kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu Namba 25 ya mwaka 2015 ikiwa na majukumu ya kusimamia na kuratibu masuala yanayohusu utumishi wa walimu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.