Man United wametuma ofa ya pound milioni 86 ikakataliwa na Juventus lakini wametuma tena ofa ya pound milioni 92 lakini mtu anayeonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ambaye bado hajakata tamaa na mpango wake wa kumpata Pogba licha ya kuwa Man United wanapewa asilimia kubwa za kumsajili.
Tayari Pogba ameripotiwa na dailymail.co.uk kukubaliana maslahi binafsi na Man United ikiwemo mshahara wa pound 200,000 kwa wiki, ila kocha wa Real Madrid bado hajakubali kuachana na mpango huo na badala yake amesema anasubiri hadi August 31 siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Pogba ambaye aliondoka Man United 2012 akiwa kacheza jumla ya mech saba katika kikosi cha kwanza, anaripotiwa kuvutiwa zaidi na mpango wa kwenda Real Madrid kuliko Man United “Kwa kipindi hiki tunashughulikia uhamisho wa Pogba kujiunga na Madrid, kwani kinaweza tokea chochote hadi August 31” Alisema Zidane

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.