ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 16, 2015

KATIBU MKUU CCM MWANZA AMSHUKIA KINGUNGE NG'OMBALE MWIRU

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana Elias Mpanda (kulia), wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza. 
*MAGUFULI KUTUA MWANZA JUMAMOSI.
*ASEMA KINGUNGE ANAFIKIRIA KWA TUMBO NA SI KICHWA. 
NA PETER FABIAN , MWANZA. 

MGOMBEA aliyechaguliwa na kupitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuri (Waziri wa Ujenzi) anataraji kuhutubia mamia ya wananchi Jijini Mwanza Julai 18 mwaka huu (Jumamosi) wakati atakapotambulishwa kwenye uwanja wa Furahisha Kirumba wilayani Ilemela jijini hapa. 

Akizungumza hii leo mbele ya waandishi wa habari, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, alisema kwamba mgombea huyo atawasili uwanja wa ndege wa Mwanza majira ya saa 8:00 mchana na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Chama na taasisi za dini na kisha kuanza msafara kuelekea uwanja wa Furahisha Kirumba ili kumtambulisha kwa wananchi wa Jiji la Mwanza na mkoa wa Mwanza. 

Mtaturu, alisema kuwa mgombea huyo atakapowasili Mwanza siku hiyo atapata fursa ya kutambulishwa na kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa mkoa huu, hii itakuwa zamu ya Mkoa wa Mwanza baada ya mgombea huyo kutambulishwa Mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Zanzibar, Mwanza kisha Mkoa wa Geita ambako anatoka mgombea. 
“CCM Mkoa tumejiandaa kumpokea mgombea ambaye Chama kimempa dhamana kubwa ya kupeperusha bendera katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu hivyo tumejianda vyema, lakini nitumie pia fursa hii kuwakaribisha wananchi wote kumsikiliza bila kujali Itkadi za vyama vyao vya siasa, ulinzi utakuwepo imara na hakutakuwa na vurugu na tunataraji Amani itawale mkutano huo,”alisema. 

Alisema kwamba, kutokana na umaarufu wa Dk Magufuri ambaye aliwahi kuwa mkazi wa Jiji la Mwanza, tunawaomba wananchi wote kufika lakini pia makundi ya kijamii ikiwemo mama lishe, waendesha pikipiki (bodaboda), wanafunzi wa sekondari, vyuo vikuu vilivyopo jijini hapa lengo likiwa ni kufanikisha mkutano huo na wananchi kumsikiliza mgombea wetu mahili. 

“Nimeshanghazwa na kauli ya iliyotolewa na Kada wa Chama chetu, Kingunge Ngombare Mwiru, aliyoitoa ya kushambulia Baraza la wazee wastaafu ambao ni viongozi wetu wa Chama na Serikali, akiwatuhumu kuendesha vikao vya mchakato wa kumpata mgombea Urais kwa mizengwe na ajenda zao za siri, wakati aliaminika na kusifika akiwa mwalimu mzuri wa siasa aliyefundisha somo hilo Chuo cha Kivukoni akisisitiza “Chama kwanza” Mtu badae inakuwaje leo anageuka hilo,”alisema . 

Mtaturu alisema kwamba kutokana na Kada huyo kumshambulia kwa maneno makali Baraza la Ushauri la wezee wastaafu anaonekana anatumika na sina budi kusema maneno yafuatayo, Mzee Kingunge “Ameanza kufikilia kwa tumbo badala ya kichwa” na anajivunja heshima yake inawezekana amesahau Ibara ya 29 inatambua wazee, hatukutarajia aendelee kusema maneno hayo kabla ya mchakato na baada ya mchakato kukamilika na CCM kumpata mgombea. 

Picha elekezi za ukutani.
Katibu mtaturu alitoa wito kwa waliokuwa wagombea kuvunja makundi yao na kumuunga mkono mgombea wa Chama hicho kutokana na kumalizika kwa mkutano mkuu, hivyo kuendelea kusema maneno ya kutaka kukivuruga Chama hicho ni utovu wa nidhamu kwani kila mwana CCM anaamini migongano humalizwa kwa njia ya vikao na kilichoshinda Dodoma ni Chama turejee kuwa wa moja “Umoja ni Ushindi”. 

Aidha amewatadhalisha watu na vikundi ambavyo vitapanga kuvuruga mkutano huo na CCM imeisha jipanga kwa ulinzi ikishirikisha vyombo vya dola, alionya kutowavumilia wanaolenga kufanya vurugu na kwamba watakaofanya hivyo wataishia mikononi mwa vyombo vya dola na pia wataonekana washamba kwa kupanga na kuvuruga amani katika mkutano huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.