NA PETER FABIAN,
BUCHOSA (SENGEREMA)
UJENZI wa Hospitali ya iliyopo Kijiji cha Isaka Kata ya Nyehunge Jimbo la Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu ameiomba serikali iharakishe kupeleka fedha za ujenzi wa Hospitali hiyo, ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
UJENZI wa Hospitali ya iliyopo Kijiji cha Isaka Kata ya Nyehunge Jimbo la Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu ameiomba serikali iharakishe kupeleka fedha za ujenzi wa Hospitali hiyo, ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
Awali akipokea taarifa ya ujenzi wa Hospitali hiyo, kutoka kwa kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema (DMO), Dr. Henry Nyamete, wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia Ilani ya Uchanguzi ya CCM na kukagua uhai wa Chama hicho.
Dr Nyamete alisema kuwa Hospitali hiyo ikikamilika itakuwa na hadhi ya wilaya na itasaidia kuondoa msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Mission Sengerema ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki, ambayo ni Teule (DDH) ya wilaya hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu, alieleza kuwa ujenzi wa Hospitali hiyo ulioanza mwaka jana, jengo la utawala la hospitali hiyo (la ghorofa moja) umefikia asilimia 80 lakini umekuwa ukisuasua kutokana na upatikanaji wa fedha kutoka serikalini kuchelewa kuja Halmashauri jambo ambalo ujenzi umekuwa na kasi ndogo.
Dr. Nyamate alifafanua kuwa, ujenzi wa Hospitali hiyo unaotarajiwa kukamilika mwaka 2016, hadi sasa jengo hilo la utawala limetumia kiasi cha Sh milioni 210 kati ya Sh milioni 560 hadi litakapokamilika huku ujenzi wa Hospitali kwa ujumla utakapo kamilika unatarajia kugharimu sh bilioni 24 .
“ Hospitali hii, ujenzi wake unahusisha wodi ya wazazi, mama na mtoto, wagonjwa wa kawaida,wanaume, chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na jengo la utawala ambalo hadi sasa limefikia asilimia 80, changamoto inayotukabili kubwa ni ucheleweshaji wa fedha kutoka serikalini,” alisema.
Aidha kukamilika kwa Hospitali hiyo mwakani itaweza kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya 400,000 wa Kata za Tarafa za Kahunda na Buchosa za Jimbo la Buchosa ikiwemo visiwa vya Kome na vingine ambavyo vinadaiwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanajishgulisha na uvuvi.
Katibu Mtaturu akizungumza baada ya kupokea taarifa na kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo mwishoni mwa wiki, Mtaturua alisema suala la Hospitali hiyo juu ya ucheleweshaji wa fedha atahakikisha analifikisha kilio cha Halmashauri ya wilaya ya Sengerema kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuuu ya Chama taifa.
“Niwapongeze kwa jitihada za ujenzi huu, pili nawapongeza kwa hatua hii mliyofikia, kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa vitendo kwani Serikali ya CCM iliyopo madarakani anaiomba iharakishe kutoa fedha ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma na kupunguza vifo vya wananchi pia mama na mtoto.” Alieleza Katibu huyo.
Naye Mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk. Charles Tizeba, ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, alisema kwamba katika kuboresha huduma za afya na kutekeleza Ilani ya Chama, amesaidia kuwezesha kupatikana magari manne ya wagonjwa na Boti mbili za kubeba wagonjwa kutoka katika visiwa hivyo vilivyopo katika ziwa Victoria.
Dk Tizeba alivitaja vituo vilivyopata magari kuwa ni Mwangika, Nyakarilo, Nyehunge na Kome kisiwani ambacho pia kilipata boti hizo na kuitaka Halmashauri na watumishi, kuvitunza ili vitoe huduma bora na iliyokusudiwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.