|
Wema Sepetu (kulia) akiwa na mama yeke Diamond mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari yenye thamani ya shilingi milioni 38.1 na mwanae Diamond Platnumz. |
INGAWA msanii Diamond Platnumz kwa sasa hayupo nchini Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni kumpa majukumu meneja wake kusimamia shughuli zote za maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mama yake naye akatimiza kama ilivyopaswa.
Ni Toyota Lexus New Model ndiyo alilo zawadiwa mama huyo ambapo Meneja Babu Tale amesema imegaharimu kiasi cha shilingi milioni 38.1 hadi kuwa na hadhi ya sasa. Mchanganuo unasema kuwa milioni 35 zimetumika kununu gari hilo ikiwa ni pamoja na kuliingiza nchini huku Milion 3.1 zikitumika kulinakshi, kuweka Music System pamoja na Seat Cover.
|
Usafiri wenyewe. |
|
Cakes. |
Zawadi ya gari toka kwa Diamond kwaajili ya mama yake imekuja mwaka huu wakati akiadhimisha umri wa miaka 55. Mama wa Diamond Platnumz amesema kuwa hakutegemea kupokea zawadi kama hiyo toka kwa mwanae, ameshukuru kwa kusema aksante huku akimwombea mwanae kwa Mwenyezi Mungu afanikiwe zaidi.
|
Kata keki tule. |
Baada ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale kwanza alitangaza utaratibu wa kuzindua video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo eneo la tukio kisha utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha kukabidhiwa gari lake.
|
Friends wa Wema Sepetu. |
|
Pamoja pix. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.