Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali vyenye thamani ya milioni 5/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulelea watoto waliokatika mazingira magumu cha New Hope Family cha Mjimwema Kigamboni (kutoka wa pili kushoto), Mlezi wa Kituo, Merry Stromberg, Victor Mshan, Anthony Mtatiro na Mwenyekiti wa kituo, Omari Kombe, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari kwa vituo vitano vinavyolea watoto hao vya Sharif Saidi Al - Bath cha Mwanza, Al- Hidaya Children's Home cha Ilala, Irishad Madrasah cha Mbezi kwa Msuguri na Kiboa Orphanage Arusha. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayuni. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.