ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 7, 2014

H BABA AKUNG'UTA VIDEO YAKE YA KWANZA MWANZA.

Msanii wa Bongo fleva toka nchini Tanzania H. Baba kwa mara ya kwanza ka-shoot kichupa chake katika mji aliozaliwa Mwanza, hii ikiwa ni mara baada ya kipindi kirefu akiitumikia sanaa yake. Unaweza usiamini lakini hiyo ndiyo hali halisi kwani video zake zote alikuwa kizifanyia kazi either jijini Dar es salaam au Nairobi nchini Kenya, Lubumbashi nchini RDC au wakati mwingine Kampala nchini Uganda. 
Akizitaja sababu za yeye kushindwa kabisa kufanya hata video moja kwa location za Mwanza, H. Baba amesema kuwa mara nyingi bajeti zilikuwa hazimruhusu kufanya hivyo (zilikuwa zikimbana) kwani ilimpasa kusafirisha mtayarishaji na timu yake, madensaz wake na timu yake ya usaidizi hivyo  ilimuwia vigumu kukamilisha yote hayo jijini Mwanza ili kupata ubora unaotakikana kwenye soko la video za kisasa.
H. Baba.
Amesema kwa sasa mara baada ya kujipanga vyema na hatimaye kupata fungu la kutosha amepata jeuri ya kufanya video ya moja kati ya nyimbo zake mpya ambazo bado hajazitoa hata katika mfumo wa audio.

Video ya wimbo TUBEBANE, itakuwa tofauti ikisapotiwa na mazingira tofauti kabisa ya miamba na nyumba za mawe za milima ya jiji la Mwanza. 
"Wakati wasanii wengine wakikimbilia nje kufanya video za nyimbo zao mimi naelekea home Mwanza kufanya kichupa, tunapaswa kutambua kuwa kinachohitajika katika utengenezaji video kwanza uwe na Mtayarishaji na Editor mzuri, pili wazo linaloweza kujenga Script nzuri, tatu msanii na timu yake mahiri yenye ubunifu pia yenye kufuata maelekezo ya mtayarishaji nne Location (mazingira ya kufanya video) na tano fungu au sapoti ya wadau wa uwezeshaji, ukiweza kuwa na yote hayo basi umewini"  Alisema H. Baba
Hizi ni pix chache tu za kichupa cha wimbo mpya wa H. Baba uitwao TUBEBANE ambao anaushoot jijii Mwanza.
H. Baba akipata baraka za wana wa home Mwanza Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.