Mchoro wa tuzo ya Mwanamakuka kama uonekanavyo pichani |
Kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa Wanawake Marafi (Unit of Women Friends).Bi Maryam Shamo akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) pamoja na Washindi wa tuzo ya Mwanamakuka 2012/2013,kuhusiana na hafla yao wanayoitarajia kuifanya siku ya Wanawake Duniani mnamo Machi,15 mwaka huu,ambayo imepangwa kufanyika ndani ya kiota kipya cha maraha na burudani,Escape One mikocheni jijini Dar,huku kauli mbiu yao wakiitanguliza kwa jila la Family Day.Pichani kulia ni Mdau mkubwa wa tuzo ya Mwanamakuka,Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania,Bi.Margareth Chacha. |
Mjumbe wa Mradi wa Mwanamakuka (Mwanamakuka Awards) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania,Bi. Margareth Chacha akisisitiza jambo mbele ya washindi wa Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 alipokuwa akiongelea siku ya wanawake Duniani tarehe 15 mwezi ujao mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Wanawake Marafiki (Unit of Women Friends),Bi Maryam Shamo. |
Pichani ni washindi wa Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 walipokuwa wamkeusanyika pamoja wakiongelea siku ya wanawake Duniani inayotarajiwa kufanyika mnamo machi 13 mwaka huu,sambamba na waandishi wa habari,mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Aidha katika siku hiyo adhimu kwa Wanawake,Umoja wa Wanawake Marafi (Unit of Women Friends),wataandaa hafla itakayowakutanisha na wadau wao mbalimbali,ambapo kaulimbiu yao itajulikana kama Family Day Kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Wanawake Marafiki (Unit of Women Friends),Bi Maryam Shamo.
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.