Huu ndiyo usafiri wetu kwa leo hapaJiji la Mwanza. |
Bajaji na Pic up zilizo na abiria zikiingia kituo cha Kemondo Nyamagana jijini Mwanza. |
Abiria wakiwa wamepakizwa kwenye moja kati ya pickup ambazo leo zimepata mwanya wa kupiga tripu jiji la Mwanza kuokoa adha ya usafiri ambayo imesababishwa na Daladala kugoma. |
Hichi ndicho kituo cha Buzuruga ambacho kinalalamikiwa na Madereva wa Daladala kuwa ni kidogo na hakikidhi mahitaji yao mpaka kipanuliwe ili magari yaweze kuingia na kutoka bila bugudha yoyote. |
Mmoja kati ya maafisa wa Tanroads akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hassan Idda (mwenye miwani) jinsi taratibu za kituoni hapo zinavyofanyika. |
Hapa ndipo Daladala hupita katika kituo kipya cha kushusha na kupakia abiria kituo cha Buzuruga jijini Mwanza kikianza kuleta nyufa kubwa. Kituo hiki kina takribani wiki moja toka |
Huu ni msingi wa Kituo hicho cha Buzuruga ambacho kimejengwa na kuanza kutumika kama wiki mbili sasa kikianza kuharibika, swali je kikimaliza miezi miwili hali itakuwaje? |
Meneja wa Tanroads Mwanza Eng: Leonard Kadashi akizungumzia hatma ya mgomo ambao umeanza leo wa Daladala na nini kifanyike juu ya kituo kilichojengwa na wakandarasi wake na kuzua utata.. |
Afisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Ziwa Eng: Japhet Ole Simaye akitoa maelekezo kwa moja ya barua kutoka Sumatra kuhusu malalamiko ya Madereva wa Daladala waliogoma leo. |
HEKA HEKA ZA MIGOMO ZALIKUMBA JIJI LA MWANZA SAFARI
HII NI WA HAICE.
MGOMO wa baadhi Wamiliki na Madereva wa magari ya
abiria aina ya Haice (Daladala) unaoendelea kuanzia majira ya saa 12:30 za
asubuhi leo Jijini hapa umedaiwa kuwa ni
batili na Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Nyamagana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo majira ya saa
11:00 za asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga ofisini kwake alisema kuwa , kufuatia baadhi
ya wamiliki na madereva kufanya mgomo wa kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi
wa Jiji hili kupitia magari yao ya abiria aina ya Haice maarufu kama Daladala
aliamua kuitisha kikao cha dharula kilicho shirikisha wadau wote.
Konisaga alisema kwamba baada ya kukaa na kusikiliza
hoja za malalamiko zilizotolewa na wamililiki na madereva hao na kuanza
kuzitafutia ufumbuzi wake ili kumaliza tatizo hilo lililopelekea kuwepo mgomo
ambapo hoja ya kwanza ilikuwa ni kupinga kukamatwa na kosa na kisha kutozwa
adhabu (Faini) pamoja na fedha lakini
wamekuwa hawapewi risti ikizingatiwa fedha hiyo inalipwa kwenye Taasisi ya
Serikali.
Alieleza kuwa hoja ya pili ilikuwa ni kuhusu
maegesho ya Haice yaliyojengwa jirani na Kituo cha mabasi cha Buzuruga kudaiwa
kuwa ni kidogo hali ambayo inapelekea magari kusubiri kwa muda huku mengi
yakiwa barabara kuu ya Mwanza-Musoma kwenye foleni hali inayosababisha askari
kuwakamata endapo wakishusha abiria wanaowahi usafiri wa mabasi na kutozwa
faini jambo ambalo wanalipinga.
Huku hoja yatatu ikiwa ni kutotambuliwa na
kuthaminiwa na serikali katika kushughulikia malalamiko yao kwa kubezwa kuwa ni
‘wahuni’ jambo lililopelekea kuwashinikiza kufanya mgomo huo ili kusikilizwa
kwa malalamiko ya kero zao juu ya taasisi za Jeshi la Polisi, SUMATRA na WAkala
wa Barabara (TANROAD) Mwanza , ambapo baada ya kikao hicho kumalizika pande
zote kwa pamoja zimekubaliana kusitisha mgomo.
“Tumekubali kuwasikiliza, lakini tumewataka
kuendelea kutoa huduma wakati tukishughulikia suala hili, tumewataka pia
kufuata sheria za barabarani na kuzingatia utaratibu uliowekwa , ambapo vituo
vya kushushia abiria visigeuzwe kuwa vituo rasmi vya kusubiria abiria jambo
ambalo huleta msongamano wa magari na wawafikishe abiria kutokana na
walivyoomba ruti na si kukatisha na kutoa tiketi kwa abiria.
Mkuu huyo alitoa wito kwa wananchi, wamiliki na
madereva wa magari ya abiria yanayotoa huduma ya usafiri kila siku nayale
ya watu binafisi kuwatolea taarifa
baadhi ya askari wachache wanaokwenda kinyume na taratibu na sheria kwa
kuwatoza fedha bila kuwapatia stakabadhi za malipo na wanaoendekeza vitendo vya
rushwa ili wachukuliwe hatua kwa vile wanalichafua Jeshi la Polisi na Serikali.
"Wito wangu wamiliki na madereva wa daladala zinazotoa
huduma ya usafiri kati ya Airport hadi Igoma-Kisesa, Bwiru hadi Kisesa na
Buhongwa hadi Airport waendelee na kutoa huduma na wasikubali baadhi ya
wanasiasa kutumia nafasi hiyo kuwahamasisha kugoma kwani ni kuwatesa wananchi
bure huku akisisitiza kuwa “Kiongozi bora ni yule anayewapenda wananchi na si
Bora Kiongozi kwani huyo yupo kwa ajili ya masilahi yake binafisi bila kujali
kuwasumbua wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.