5th
Julai 2013
Bismillah-ir-Rahman-ir-Rahim
Mh. Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Msaafu,
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
CCM,
na Mbunge wa Monduli, Edward
Lowassa (MB)
Kaimu Mkuu wa Mkoa, Mwanza
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza
Waheshimiwa
Masheik,
Maimamu
na viongozi wote,
Waheshimiwa
Waalikwa
ASALAM
ALAIKUM
Bwana
Yesu Asifiwe
Tumsifu
Yesu Christu
Ni heshima kubwa kwangu kuwakaribisha nyote
kwenye hafla yetu ya leo ya kuchangia uboreshaji na upanuzi wa matangazo ya vituo
vyetu vya redio, Iqra FM na redio Sauti
ya Qur-ani.
Ninajua kuwa haikuwa rahisi kwako kukubali
mwaliko wetu kutokana na shughuli zako nyingi, lakini kutokana na moyo wako wa
kujali shughuli yoyote ya maendeleo, umekubali kuwa nasi leo.
Kwa kuzingatia nimekuwa nikijihusisha kwa hali
na mali katika kuendeleza shughuli za kituo hiki cha Iqra FM na shughuli
nyingine za kijamii, nikiwa mlezi wa JUQUSUTA taasisi inayosimamia redio hiyo,
nakumbusha tarehe 5 Decemba 2012 nilikua mgeni rasmi katika shuguli ya kutafuta
pesa kwa lengo la kufanikisha upanuzi wa redio Iqra na redio Sauti ya Qur-ani ni
furaha kubwa kwangu kuona wewe mgeni rasmi, na wanajamii wengine wakijitokeza
kusaidia kufikia lengo la kuboresha shughuli za vituo hivi.
Ninawashukuru sana, kwa ukarimu wenu.
Kazi ya kuboresha shughuli ya kituo cha redio
cha Iqra FM inakadiriwa kugharimu , Shilingi 386,930,000 (milioni mia tatu na
themanini na sita na laki mia tisa na thelathini) na redio ya Sauti ya Qur-ani
shilling 250,000,000.00 (million mia mbili na hamsini).
Kazi hizi ni pamoja na kujenga minara za
matangazo, kupanua vituo vya Iqra FM na Sauti ya Qur-ani, na ujenzi za studio
ya kisasa.
Ninaamini
Maadili ya Uislamu ndio msingi muhimu wa kila muumini wa dini ya Kiislamu katika
maisha yake ya kila siku na katika shughuli yeyote aifanyayo.
Ninaamini vituo
vya redio Iqra FM na redio Sauti ya Qur-ani kitaonyesha Uislamu kama dira
unayohusisha mambo yahusuyo jamii. Ni cheche ya kimungu ambayo inatoa ubinafsi
pia inayo waunganisha binadamu katika jamii moja. Korani inasema binadamu
ameumbwa kutokana na roho moja, kama mwanaume na mwanamke, jamii na mataifa,
ili watu waweze kufahamiana. Inawaleta watu wa imani zote kwenye jukwaa moja,
kwa kupitia wema.
Na jioni
hii, sisi sote tuko kwenye jukwaa moja kwa kupitia wema.
Vituo hivii vikiboreshwa na kupanua matangazo
yake vitaweza kuwafikia wasikilizaji wengi zaidi, wakiwemo Waislamu na
wanajamii wengine, na wataweza kupata
mawaidha na taarifa zitakazo wa wezesha kuwa wacha Mungu na raia wema wa nchi
yao.
Vituo vya Iqra FM na Sauti ya Qur-ani vikiwa ni vituo
yya Kiislamu vina wajibu mkubwa wa kujenga maadili ya Kiislamu miongoni mwa
Waislamu na kujenga mahusiano mema kati ya Waislamu na wanajamii wengine.
Kuwa na mawazo
mbadala ni nguvu katika jamii, na siyo udhaifu kwenye jamii. Kwa bahati nzuri
majibu yote ya kiroho na kidunia tunayapata kutoka kwenye Quran Tukufu na
maisha ya Mtume Mohamed.
Kwa maana hiyo naipongeze JUQUSUTA na BAKWATA kwa
kazi nzuri ya kuendeleza maadili ya kiislamu katika jamii.
Mheshimiwa mgeni rasmi, bila shaka sote
tunafahamu kuwa vyombo vya habari, hususan vituo vya redio, ni muhimu katika
kuelimisha jamii, kuihabarisha na kuiburudisha.
Aidha, katika
matangazo yake, itakuwa vyema vituo vya Iqraa FM na Sauti ya Qur-ani, vitakuwa na
vipindi ambavyo vinatoa mwanga
kuhusu madhehebu mengine ya kidini,
lakini bila kuya kashifu.
Mimi ninaamini
kwamba kiongozi bora ni yule ambaye anajenga na siyo anayebomoa, Mheshimiwa mgeni rasmi, wewe kama
kiongozi shupavu na makini unaendelea kujenga jamii kwa ukarimu wako kwa
kuchangia kwa hali na mali , shule,
vyuo, misikti , makanisa n.k.
Naomba niwashukuru awali wale wote
watakaokuunga mkono leo ili uweze kuviwezesha vituo hivi kufanya kazi zake.
Nawambia
toweni kwa ajili ya mungu, mungu atawalipa maradufu.
Upo
msemi usemao – na nina nukuu
‘(FANYA YA MUNGU – MUNGU NAE ATAFANYA YAKO’)
Mwisho wa kunukuu.
Leo,
tutaraji Mungu nae kutufanyia makubwa katika maisha yetu, shuguli za kila siku na
afya zetu, amen.
Mh.Mgeni
Rasmi, kwa
pamoja tusiache kuiombea nchi yetu Amani,
Utulivu, Mshikamano Na Kuvumiliana.
Mh. Mgeni Rasmi
ninahamu sana, sasa, kufaidika na fikra na busara zako ili tujenge taifa letu
sote kwa pamoja.
Sala yangu ni
kwamba Mungu awe nawe, akuimarishe afya yako, akupe moyo na uwezo wa kuongoza
kwa hekima zaidi.
Tumuunge
mkono mgeni wetu, tuchangie kwa moyo wetu na uwezo wetu, ili tupate Baraka za
Mungu wote.
WABILLAHI
TAUFIQ
Asanteni.
Baada ya kumalizika harambee
hiyo ndipo Mwenyekiti wa Kamati ya harambee hiyo Sheikh Hassan Kabeke alitoa
taarifa ya fedha zilizochangwa awali na zile zilizopatikana ambapo jumla kuu kilikuwa
kiasi cha shilingi milioni 590.8 na kuelezwa kuwa kiasi hicho tayari kilikuwa
kimevuka lengo lililowekwa la milioni 500 na kamati yake.
Katika harambee hiyo wachangiaji
wakubwa waliojitokeza ni MNEC wa Tarime Christopher Gachuma (ml.10), MNEC wa
Arumeru Mathias Manga (ml.10), Kampuni ya MOIL Mkurugenzi Altaf Mansoor
‘Dogo’(ml.10),Kampuni ya GBP (ml.15) Mbunge Ezekial Maige wa Msalala (ml.2),
MNEC wa Busega Raphaer Chegeni (ml.2).
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja (ml.2), Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hida Hassan
(ml.3), Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (ml.1), Salum Mbuzi Mbuge wa
zamani wa Meatu (ml.6), Mussa Muzia (B.O.T) ml.2, Barnabas Mathayo (ml.2), MNEC
wa Musoma Vedastus Mathayo (ml.2) huku Lowassa akifunga dimba kwa kuchangia
milioni 20 tasilimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.