ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 24, 2012

MBUNGE WA RORYA ASHIRIKI UZINDUZI WA HOTEL FREDITO INN NDANI YA KIJIJI CHA KOWAK

Mbunge wa wilaya ya Rorya mkoani Mara Mh. Lameck Airo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kowak waliojitokeza kwa wingi ndani na nje ya ukumbi kushuhudia uzinduzi wa hoteli mpya iitwayo Fredito Inn iliyojengwa kisasa ndani ya kijiji hicho kwa madhumuni ya kutatua uhaba wa vyumba vya wageni na huduma madhubuti za kihotelia zinazoikabili eneo hilo kwani ni mara nyingi wageni wanapo fika eneo hilo au kata jirani hukumbana na kadhia ya kukosa vyumba kwaajili ya kupumzika na wengi wamekuwa wakisita kutembelea kijiji hicho kutokana na uhaba wa huduma,  hivyo ujio huu utalifanya eneo hili kupata maendeleo kwa watu aina mbalimbali kutembelea.  Mwisho mbunge Airo aliwasihi wadau wengine walioko mikoa ya mbali kuwekeza Nyumbani.

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Lady Morine na bendi yake walipiga bonge la show sijawahi ona duniani.

Mara baada ya mgeni rasmi Mh. Mbunge kukata utepe na kuingia ukumbini nafasi ya mmiliki wa Hoteli Fredito Inn Bw. Fredito (kulia) alipata nafasi ya kutoa shukurani zake akiwa na mkewe jukwaani, kushoto aliyenyanyua mkono ni mc wa shughuli Bw. Kiche Makoa.

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Lady Morine na bendi yake walifanya makamuzi ya hatari ndani ya uzinduzi wa Hoteli Fredito Inn ndani ya kijiji cha Kowak kilichopo Utegi wilayani Rorya mkoani Mara.

Show time na mmoja kati ya madensa safu ya bendi ya Lady Morine kutoka nchini Kenya.

Askwambie mtu ilikuwa kiboko.

Mpaka chini..

Wanakijiji nao wamo...

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Lady Morine na bendi yake akiimba moja kati ya vibao vyake ambapo ngoma ilipigwa mpaka mida ya miswaki na kusitishwa pale nyomi ya watu waliokuwa nje ya ukumbi kung'ang'ania kutinga ndani kushuhudia burudani.

Mdau away from dar to this area akinasa matukio.

Si kwa macho tena bali kitu ng'adu kwa ng'adu ..sasa ni zamu ya wananchi kula burudani ya mutu na mutu.

Wadau wa ukweli toka mikoa mbalimbali hapa nchini nao walihudhuria tukio hili lenye nia ya kufanya maboresho ya kijiji cha Kuwak kuwa na vivutio kwa wageni kutembelea kutoka kushoto ni Ayuni Ayuni, Salvin Musa, Solomon Mirondo na Josephine Mirondo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.