ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 23, 2012

MBUNGE WA RORYA MH. LAMECK AIRO, ATOA MSAADA KWA MTOTO ANAYESUMBULIWA NA SARATANI YA MENO KIJIJI CHA KIROGA.

Pichani Mbunge wa Wilaya ya Rorya Mh. Lameck Airo (mwenye suti nyeusi na kofia nyeupe) akidadisi hali ya mtoto Victor Chuki mara baada ya kufanya mazungumzo na Bw. Chuki Eliaki Modudo ambaye ni baba wa mtoto huyo wa kwanza (kushoto).
 ILI kuokoa Afya na Maisha ya mtoto Victor Chuki anayesumbuliwa na saratani kwenye meno iliyo sababisha uvimbe kwenye shavu na meno kung’oka bila utaratibu, hatimaye mbunge wa Rolya Mh. Lameck Airo ametoa msaada wa fedha za safari, kujikimu na huduma zote za matibabu kwaajili ya kufanikisha kuirejesha afya ya motto huyo.


Mh. Lameck Airo ametoa msaada huo katika kijiji cha Kirogo wilayani Rorya mkoani Mara, ambapo gharama halisi itajulikana mara baada ya kukamilika matibabu ya mtoto huyo ambaye ataambatana na mzazi wake (baba wa mtoto huyo) Bw. Chuki Eliaki Modudo, hadi hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza alikoahidiwa na wataalamu wa tiba kwaajili ya kupata matibabu na kama kutakuwa na  ulazima wa kuhamishiwa Hospitali nyingine kwa matibabu zaidi mbunge huyo ameahidi kubeba dhamana hiyo kuhakikisha mtoto huyu anapata tiba.
Mtoto Victor Chuki (5) ugonjwa huu kwake ulianza kwa uvimbe, baada ya siku chache akaanza kutema mate kila saa, jino likang'oka bila kuwa na maumivu, kisha jino jingine, wazazi wake kuona hali si shwari wakampeleka hospitali ya Shirati ambapo walipewa maelekezo kwenda hospitali ya wilayani Tarime kwa mganga wa meno hapo alipewa walipewa maelezo kuwa tatizo hilo ni geni kwao hivyo waelekee hospitali ya Bugando au Muhimbili.

Mtoto Victor Chuki akiwa na baba yake Bw. Chuki Eliaki Modudo mara baada ya kupewa fedha za nauli na kujikimu ambapo watafunga safari kuelekea jijini Mwanza kutoka kijijini hapa, na watapokewa na mbunge huyo kwaajili ya matibabu zaidi hospitali ya Rufaa Bugando.
Bofya play KUSIKILIZA KISA KIZIMA

Mtoto Victor Chuki (5) kwamujibu wa kauli zake anasema kuwa ukimshika shavu hasikii chochote (eneo la shavu limekufa ganzi) hata ukifinya hasikii maumivu, meno ya upande huo wa uvimbe yamepukutika wala hawezi kutafuna kupitia upande huo, ni muda wa mwaka sasa akitaabika na hali hii.  

Cheti cha vipimo toka kwa daktari, ingawa kimeonesha umri wa miaka 7 lakini kwa mujibu wa mzazi wa Victor, mtoto huyu amaumri wa miaka mi 5 mwaka kesho atatimiza 6.  

Blogu hii inampongeza hatua hii ya mbunge wa jimbo hili vilevile inaisihi jamii kuwa na moyo wa kujitolea kama ilivyoonyeshwa na Mh. Mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.