Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ernest J. Mangu akizungumza na wandishi wa habari (hawako pichani) leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za jeshi la polisi mkoa wa Mwanza. |
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza katika kuhakikisha kuwa wananchi
wanasheherekea vyema sikukuu ya Christimas na Mwaka mpya katika hali ya amani
na utulivu, limepanga mikakati madhubuti ya kupambana na uhalifu na wahalifu
katika ngazi zote kuanzia visiwani na vitongoji, vijiji, wilaya na mkoa kwa
ujumla.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ernest J. Mangu amesema kuwa katika kipindi chote cha sikukuu
ulinzi utaimarishwa katika maeneo yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko ya watu
kuanzia katika maeneo ya starehe, sehemu za ibada, aidha wamiliki wenye vyombo
vya usafiri wanakumbushwa kuzingatia wajibu wao wa kufuata sheria zote za
usalama barabarani.
Kuhusu hali tete ya usalama na matukio ya uvamizi yanayo ripotiwa kila
kukicha toka maeneo ya visiwa vya mkoa wa Mwanza hususani la utekaji wavuvi
lililojitokeza hivi karibuni kwenye kisiwa cha Ukerewe, Kamanda amesema kuwa
jeshi lake limeongeza vikosi vya askari polisi na kwa kushirikiana na wamiliki
wa vyombo vya usafiri majini jeshi la polisi litaendesha doria ziwani muda
wote.
BOFYA PLAY UMSIKILIZE.
BOFYA PLAY UMSIKILIZE.
Pia wazazi wamekumbushwa kuhakikisha kuwa watoto wadogo wanakuwa
na watu wazima wa kuwaongoza barabarani.
Aidha Kamanda Mangu amewataka wazazi na wananchi kwa jumla
kutowaruhusu watoto wadogo kushiriki kwenye mikusanyiko ya usiku kwa mfano baa
na kumbi za starehe kwani ni watawaepusha
na mawaa yanayoweza kujiri na kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Kwa
wamiliki wa kumbi za starehe wamekumbushwa
kuzingatia kuingiza watu katika kumbi za starehe kulingana na idadi ambayo
kumbi hizo zinastahili ili kuepuka misongamano ya watu inayoweza kuleta maafa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.