MEYA wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula, amemtembelea na kumjulia hali majeruhi Chacha Ryoba (29) mkazi wa mtaa wa Pamba Jijini Mwanza aliyepigwa risasi na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akipatiwa matibabu baada ya kutokea vurugu kati ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) na askari mgambo wa Jiji la Mwanza katika eneo la stendi ya zamani ya Tanganyika mwishoni mwa juma lililopita Wilayani Nyamagana Jijini hapa.
Hatua hiyo ya kumtembelea majeruhi huyo imekuja mara baada ya kijana huyo kuwa mhanga wa vurugu hizo.
Mstahiki Meya ameweza kumchangia gharama za matibabu kiasi cha shilingi laki mbili na nusu (250,000/=) kijana Chacha ili kuwezesha kufanyiwa upasuaji katika mkono wake wa kulia kuondolewa vipande vya mabaki ya risasi baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo ambapo mtu mmoja alikufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa akiwemo kijana huyo
Pia msafara wa Mstahiki meya ulimtembelea Bw. Juvenile Matagili (kushoto) ambaye ni mratibu wa Chama cha Umoja wa Wavuvi mkoani Mwanza (TAFU) ambaye anapatiwa matibabua ya mifupa kwenye hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Mazungumzo kabla ya kuondoka hospitalini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.