ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 11, 2012

MBWANA SAMATA NA VICTOR WANYAMA NDIYO HABARI YA MJINI KUELEKEA MECHI YA TAIFA STARS NA HARAMBEE STAR


Harakati za usafi na matayarisho zinaendelea kwenye dimba la CCM kirumba kwa ajili ya kuwalaki wapenzi wa soka watakao shuka toka viunga mbalimbali vya jiji la Mwanza, mikoa mingine toka kanda ya ziwa kama vile Shinyanga, Geita, Mara, Kagera na Simiyu kushuhudia mechi ya kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA baina ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Star) mchezo unaotajwa kuwa utakuwa na msisimko wa aina yake.

Uwanja huu unanyasi halisi ambazo kwa ufupi  ni sehemu ya sifa ya ziada ya kujivunia kwa wakazi wa Kanda ya ziwa.


Ni nani kulisulubu lango hili ambalo linatajwa kuwa huwa halilali na njaa...?


The pich...


Shughuli za usafi zikiendelea...


Kimiani......


Hatua za mwisho mwisho ambapo Taifa Stars wao wanatarajiwa kuingia jijini Mwanza leo jioni, na kuanza mazoezi kesho.


Ni nani atakosa kuwa sehemu ya jumuiko litakalo kuwa hapa CCM Kirumba? Kwani hii ni historia nyingine kusogezewa mechi ya kimataifa inayo lihusu taifa letu, mechi itakayo hudhuriwa na si mashabiki tu wa soka wananchi wa kawaida wa Tanzania bali viongozi wa Serikali na vyama mbalimbali vya siasa nchini pamoja na watu kutoka nchi mbalimbali Ukanda wa Afrika mashariki za Kenya (wageni wetu), Uganda, Rwanda na Burundi hasa ukizingatia kuwa Mwanza ni mji mkuu wa biashara na nikiunganishi cha mataifa hayo ya maziwa makuu.

Huyu jamaa ni mzoefu ....


Wadhamini wa Taifa Stars Kampuni ya Bia Tanzania TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager wakiweka mabango yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.