ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 20, 2012

KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI YAZINDULIWA RASMI JIJINI MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya uzazi salama inayojulikana kwa jina la Wazazi nipendeni iiyozinduliwa rasmi leo katika uwanja wa Nyamagana ambapo kampeni hiyo inahamasisha mama wajawazito na wenzi wao kuchukua hatua muhimu kuhakikisha ujauzito wenye afya na uzazi salama.

Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau wa afya mbele ya bango kubwa la kampeni iliyozinduliwa leo jijini Mwanza ya uzazi salama ijulikanayo kama 'Wazazi nipendeni' 

"Leo tunasherehekea mama wajawazito kama kauli mbiu ya kampeni inavyosema "Wazazi Nipendeni ulinzi mnaonipa ndio tumaini langu" Hii kampeni itatumia Runinga, Radio,Mabango makubwa ya matangazo ya biashara na machapisho yatakayoshirikisha uzazi wa mpango wa mtu binafsi ambao mama mjamzito na wenzi wao wanaweza kutumia kujiandaa kwaajili ya kujifungua" Alisema Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo waakihutubia 

Bi Alisa Cameroon Mkurugenzi wa Afya wa U. S Agency for International Development (USAID) akizungumza na kusanyiko lililojitokeza leo kwenye viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza kuzindua kampeni ya 'Wazazi Nipendeni'.

Wanawake wote wajawazito na wale waliojifungua hivi karibuni kutoka kanda ya ziwa ambao wamethubutu kufika kwenye viwanja vya Nyamagana wamepatiwa huduma wanazohitaji za Afya zao na watoto wao pamoja na ushauri kupitia kampeni ya 'Wazazi nipendeni'.

Vile vile kwenye eneo hili kulikuwa na utaratibu wa kuchangia damu salama uliosimamiwa na wadau wa Afya toka Hospitali ya Agha Khan ya jijini Mwanza.

Mpango wa damu salama ukiendelea viwanjani hapa.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo pia alipata fursa ya kuzindua kitabu maalum chenye maelezo tosha juu ya Kampeni hiyo ya kulinda Afya ya mama na mtoto.

Kitabu chenyewe ndiyo hiki.....

Katibu mkuu wizara ya Afya Bi. Regina Kikuli akihutubia hadhira iliyojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya 'Wazazi Nipendeni' ambayo inaongozwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii sehemu ya Uzazi na Kitengo cha Uratibu wa Afya ya mtoto pamoja na program ya Taifa ya kudhibiti Malaria (NMCP), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), mpango wa kukuza Afya na sehemu ya Elimu na ushirikiano wa mashirikia yote ya Afya ya Umma na binafsi.

Wadau wa kampeni hiyo ndani ya kusanyiko la leo viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza.

Menejimenti ya wadau wa Agha Khan.

Huduma ya bure kwa Afya ya mama na mtoto ndani ya mpango wa 'Wazazi Nipendeni'

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.