ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 19, 2012

MWANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA WAINGEREZA KUKUZA MICHEZO

Afisa wa Idara ya michezo mkoa wa Mwanza James ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wa kupokea mradi wa kukuza michezo unaofadhiliwa na Uingereza akifungua kikao cha kuzindua mradi, pembeni yake aliyeketi ni Afisa Mwendeshaji wa Michezo Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo Mohamed Kiganja.

Baadhi ya wadau wa michezo mkoani Mwanza wakisikiliza kwa makini yanayojiri ndani ya kikao cha Mradi wa Michezo kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza ambapo jiji hili pekee lenye michezo zaidi ya 14 inayochezwa limebahatika kuwa kitovu cha uendeshaji wa mradi wa kuendeleza michezo unaofadhiliwa na nchi ya Uingereza.

Afisa Utamaduni wa jiji la Mwanza mama Makenke (wa kwanza kulia) akiwa na wadau wengine wakisikiliza  kinachojiri kwenye uzinduzi wa mradi huo wa Michezo uliogawanyika sehemu zipatazo tano ikiwa ni pamoja na Sehemu ya wanawake Uongozi, Mafunzo kwa makocha, Mfumo wa kukuza vipaji vya watoto katika michezo na utambuzi, Riadha, Vollebal na Soka.

Afisa Michezo mwandamizi kutoka Baraza la Michezo ambaye vilevile ni Mratibu wa mradi wa Michezo unaofadhiliwa na Uingereza akitoa maelekezo juu ya namna mradi huo utakavyonufaisha jamii  na taifa kwa ujumla.


Afisa Mwendeshaji wa Michezo Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo Mohamed Kiganja.


Uingereza kupitia mwakilishi wao waliyemtuma kwenye Kabinet ya Olimpiki ya kuwania uandaaji wa michezo mikubwa ya Olimpiki, Sebastian Cole, walishinda kuandaa mashindano hayo yaliyofanyika mwaka huu nchinimwao kupitia ahadi ya sera yao iliyowapatia kura nyingi kwamba Iwapo watapewa dhamana ya kuandaa mashindano hayo mwaka 2012 basi Inchi hiyo Itashanifisha michezo kwa jamii.

Nayo ilishinda kwa kura nyingi ikiishinda Ufaransa, hivyo basi hatua hizi ni sehemu ya utekelezaji miradi ya ahadi ya Uingereza kwa nchi walizozichagua zipatazo 20 ikiwemo Tanzania iliyobahatika kutoka nchi tofauti za mabara tofauti hapa ulimwenguni.

Uingereza wamedhamiria kuwafikia watoto wenye vipaji wapatao milioni ishirini kwenye mradi.

Mradi huu haukukosea kuangukia jijini Mwanza kwani mkoa huu una hazina ya miundo mbinu kama vile vyuo vya  michezo ambapo kuna Chuo cha Malya kinachofanya Training ya Makocha, Chu cha Ualimu Butimba kinachotoa pia Waalimu wa taaluma ya michezo na Chuo cha ualimu Umulutungulu ambacho Serikali imeamua kukiboresha ili kuendana na ufundishaji waalimu taaluma ya Michezo mikakati ikiwa imekwishaanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.