Monday, November 19, 2012
|
Mkuu wa Kitengo cha Uzazi toka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Koholeth Winani akifungua kampeni ya uzazi salama Mwanza ijulikanayo kwa jina la Wazazi Nipendeni ambapo kupitia kampeni hiyo itasaidia kupunguza vifo vya mama wajawazito barani Afrika na Tanzania.
Kwa muda wa siku mbili kuanzia leo ndani ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza akina mama wajawazito pamoja na wenzi wao wanakutana kupata huduma ya kliniki BURE kwa nia ya kutambua afya zao na kupewa elimu mbalimbali za Afya ya mama na mtoto. |
|
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali wakiwa wamejumuika na wataalamu kutoka mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yanayoendesha kampeni hiyo kwa ushirikiano ili kulinususru taifa kwani kiwango cha mama wajawazito wanaofariki nchini Tanzania ni kikubwa 454 wanakufa kila uzazi wa watu 100,000, na watoto 26 wanakufa kati ya 1000 wanaozaliwa, na kiwango cha watoto wachanga wanaofariki ni 51 kwa kila 1000 waliozaliwa hai. |
|
Kampeni ya Wazazi Nipendeni imelenga kutekeleza CARMMAT kwa kuwawezesha mama wajawazito na wenzi wao kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya ujauzito wenye Afya na uzazi salama, kampeni ikijumuisha maeneo yote ya Afya ya uzazi salama, kama kuwahi kuanza kliniki na kuhudhuria kliniki, kujikinga na malaria, kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto HIV (PMTCT), mpango wa uzazi kwa mtu binafsi na uzazi salama. |
|
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukuwa taarifa kwaajili ya vyombo vyao ka maslahi ya wananchi. |
|
Kampeni ya 'Wazazi Nipendeni' licha ya kutumia vyombo mbalimbali vya habari katika kufikisha ujumbe kama vile Radio, Televisheni, Magazeti, Mabango makubwa, Machapisho na mitandao katika kufikisha elimu ya uzazi wa mpango wa mtu binafsi ambao mama wajawazito na wenzi wao wanaoweza kutumia kujiandaa kwa ajili ya kujifungua kampeni hiyo sasa imekuja na mpango wa kufikisha ujumbe kwa njia ya UJUMBE MFUPI WA SIMU yaani SMS.
Mama wajawazito, mama wenye watoto wadogo wa umri wa wiki 16 na wanaowasaidia walituma neno MTOTO kwenda namba 15001 bure bila kulipia ambapo mara baada ya kusajiliwa watatumiwa ujumbe wa maneno bure ambao unahusu mimba salama na huduma za awali kwa mtoto mchanga. |
Wazazi Nipendeni inaongozwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii sehemu ya uzazi na kitengo cha uratibu wa afya ya mtoto pamoja na program ya Taifa ya kudhibiti Malaria (NMCP), Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi (NACP), kampeni inafadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia mawakala wa maendeleo wa kimataifa (USAID), mpango wa kudhibiti malaria wa rais wa U.S.A (PMI) mpango wa dharura wa rais wa Marekani kudhibiti Ukimwi (PEPFAR) pamoja na kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC)
|
"The unique SMS service offers the registrants time sensitive reminders for ANC visits, SP doses for preventation of malaria ina pregnancy as well as information on testing for HIV, nutrition, individual birth planning and much more" Says Sarah Emerson Country manager of Mhelth Tanzania Partnership for tah CDC Foundation. |
|
Muuguzi wa Afya ya mama na mtoto toka hospitali ya Agha Khan Bi. Celestina Nyenga, akitoa ufafanuzi juu ya huduma ya BURE ya Ujumbe mfupi kupitia simu itakavyo rahisisha mpango wa kuboresha afya za akinamama wajawazito nchini bila usumbufu. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.