ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 3, 2012

TAPELI LAJISALIMISHA LENYEWE POLISI KUKWEPA KIPONDO CHA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.

Video ya tukio.

 Jamaa mmoja ambaye jina lake halikupatikana anayesadikika kuwa ni tapeli mchana huu kashushiwa kipondo na wananchi wenye  hasira kali mara baada ya yeye na wenzake kufanikiwa kumtapeli mfanyabiashara mmoja maarufu jijini hapa wakifanya biashara naye na kumlipa makaratasi na si fedha halali yaani dola za kimarekani kama makubaliano yalivyokuwa.


 Akiwa na wenzake huku wakitumia usafiri wa gari aina ya Noah yanye namba za usajili za Uganda (bahati mbaya hazikunukuliwa) Tapeli hilo (pichani) mara baada ya kukamilisha kufanya biashara na tajiri huyo kuwapatia mali, Matapeli hayo yaliondoka eneo la biashara huku wakimwacha tapeli mwenzao aliyepichani hatua chache toka eneo la tukio ili asome harakati za mfanya biashara huyo pindi atakapostukia kuwa kapewa makaratasi ya kimazingaombwe na si za  madolali kama halali ya malipo.

Waliposepa wazeeya, yule Mfanyabiashara maarufu akagutukia mchezo ingawa alikuwa kisha chelewa kwani matapeli wengine walikwisha timua eneo la unoko.

Angaza huku na kule ...mara nkabaaaaa jicho likamnasa mmoja aliyewaona nao... mfanyabiashara akakusanya washirika wenzake ... mara tip ... tapeli aliyekuwa akichungulia msala akanaswa na kuanza kuchezeshwa kichapo. 
Ni daftari lililokatwa kiufundi saizi ya dola za kimarekani
 Wengi wafanyabiashara hususani wa samaki na wavuvi wamekwisha lizwa na matapeli hao jijini hapa wakibamizwa na biashara za dhahabu feki, almasi feki na mitindo mingine ya kubadilisha fedha za madafu kwa dola za Kimarekani.
 Makaratasi hayo yalikuwa yameviringishwa vizuri kwenye karatasi ya kaki na kuwekewa raba bendi mtuno wake mithili ya fedha.

 Mashambulizi huku jamaa huyo akitafuta njia kujinasua mikononi mwa wenye hasira.

 Akikimbilia kwenye gari la maafande waliokuwa na safari zao kuelekea lindoni..

 Dushwaaaa... akajitumbukiza kujisalimisha....

Vuta pumzi 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.