ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 2, 2012

MEYA WA JIJI LA MWANZA AHUDHURIA MAAFALI YA NNE SHULE YA SEKONDARI NYAKULUNDWA

Baada ya kuwasili eneo la shule ya sekondari Nyakulundwa iliyopo kata ya Mkuyuni wilaya ya Nyamagana jijini  Mwanza, Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alivikwa skafu na skauti wa shule hiyo ikiwa ni ishara ya kuwa mgeni rasmi kwenye maafali hayo.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maafali  ya nne ya shule ya Sekondari Nyakulundwa huku akishuhudiwa na Mkuu wa shule hiyo (kushoto) na diwani wa kata ya Mkuyuni Lugo Fashion (kulia). 

Wageni na ndugu wa wahitimu katika eneo lao maalum.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nyakulundwa wakishuhudia maafali ya ndugu zao.

Sehemu nyingine ya baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nyakulundwa wakishuhudia maafali ya ndugu zao.

Wanafunzi wa shule ya msingi Nyakulundwa pia walikuwepo eneo la tukiokushuhudia kaka zo wakihitimu.

Wahitimu wa Shule ya Sekondari Nyakulundulwa wakiwasili eneo la viwanja vya maafali ili kukabidhiwa vyeti.
Ni akati wa Risala ya Maendeleo ya Shule ya Sekondari Nyakulundulwa iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyakulundulwa akitoa nasaha zake sambamba na kumkaribisha mgeni rasmi Mstahiki Meya kujibu risala.








Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.