ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 30, 2012

MAONYESHO YA BIASHARA YA TCCIA 2012 SAFARI HII KUFANYIKA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA VIWANJA VYA NYAMAGANA

Maonyesho ya saba ya EastAfrica Fair yanayoandaliwa na TCCIA Mwanza yanataraji kuanza rasmi  tarehe 31/08/2012  mpaka tarehe 9/09/2012 katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza yakihusisha makampuni mbalimbali ya bidhaandani na nje ya nchi.

Maonyesho hayo yatatoa fursa kwa makampuni yaliyo ndani ya Tanzania na nje kuwa yapo na yanajihusisha na usambazaji au uzalishaji wa bidhaa aina gani pia jumuiya za wafanya biashara kupata fursa ya kuanzisha mitandao katika dhana ya usambazaji bidhaa.

Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali wakichukuwa taarifa.

Hii ni fursa ya wakazi wa Mwanza kujifunza jinsi ya kuboresha bidhaa zao kupitia ushindani,kujifunza jinsi ya fursa zilizopo kwenye masoko ya nje na jinsi ya kuyatumia. 

Washiriki watatoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, maonyesho ya mwaka jana yalihudhuliwa na watazamaji takribani laki nne na matarajio mwaka huu ni kuwa na watazamaji  laki sita.  Kauli mbiu ya Maonyesho haya ni  Tumia fursa zilizopo ndani ya soko la Afrika Mashariki.

Bidhaa na huduma zisizoruhusiwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Silaha za aina zote, Risasi, Mizinga (Bidhaa za kivita), lakini vilevile hawategemei kuwa na huduma za masuala ya  kisiasa na kidini kwani ni Biashara na Uwekezaji tu ndiyo umezingatiwa na kamati ya maandalizi

Siku ya jumanne tarehe 4 september Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi na Mh.Abdalah Kigoda ambaye ni Waziri wa Viwanda na Masoko nchini Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.