ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 1, 2018

NBC TAWI LA MWANZA WATAMBULISHA RASMI HUDUMA YA KIKUNDI MOBILE KATIKA KUHITIMISHA WIKI YA WATEJA



GSENGOtV




Vyovyote iwavyo, maisha lazima yaendelee licha ya changamoto zitakazojitokeza katika safari hiyo. Bila kujali umri, kila mmoja anayo malengo anayokusudia kuyatimiza.
Kati ya mambo yanayowakabili vijana ni namna ya kukabiliana na maisha kiuchumi. Jambo hili linatokana na ugumu wa kuajiriwa au kujiajiri. Kutokana na ugumu wa kuajiriwa, wahitimu wa ngazi mbalimbali hutafuta ajira hasa rasmi lakini wanapozikosa, kama mbadala wa kuajiriwa, baadhi hulazimika kujiajiri.
Hata hivyo wapo wanaoamua kutoajiriwa badala yake kujiajiri hata kama wanapata kazi za kuajiriwa.
Pia wapo waliowahi kuajiriwa lakini wakaacha na kujiajiri au kuchanganya kuajiriwa na kujiajiri. Vijana wengi wanakumbana na changamoto kubwa katika azma ya kujiajiri. Kubwa ni upatikanaji wa mtaji.
Kwa kuliona hilo baada ya kumalizika kwa wiki ya mteja, Benki ya NBC Tawi la Mwanza imezindua huduma ya Kikundi Mobile kwa wateja wake wote wenye akaunti ya kikundi ili kurahisisha upatikanaji wa miamala kwa wanakikundi wenye akaunti NBC bila kufika tawini.













Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.