Ni kipindi kirefu sasa Mkurugenzi wa Uzalishaji Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba hajaonekana hadharani, sasa chombo hicho cha habari leo November 20, 2018 kimetoa taarifa kuhusu kiongozi huyo.
Seba Maganga kutoka CMG amesema kuwa Ruge kwa sasa hayupo kazini kutokana na kuumwa hivyo amepatiwa muda wa kupumzika hadi pale atakaporejea kwenye hali yake ya kawaida.
"Katikati ya May kuelekea June ya Mkurugenzi haikuwa nzuri na akatuomba kupata muda kidogo ili ashughulikie afya yake na tuliona hili litakuwa dogo tu na tukatoa baraka zote. Lakini ripoti za kitabibu zikasema muda wa kupumzika ni mdogo hivyo akaongezewa muda," amesema.
"Madaktari wanakiri Kiongozi wetu ni mpambanaji na bado anahitaji muda wa kupumzika na ni kweli hizo changanoto zilikuwepo," ameeleza Seba.
Kwa hatua nyingine Seba amesema kuwa Rais Dkt John Magufuli alipopata taarifa za hali ya kiafya ya Ruge Mutahaba alisikitika sana na aliamua kumshika mkono kama baba afanyavyo kwa mwanaye wa kumzaa.
"Tunamshukuru Rais kutokana na yeye mara baada ya kupata taarifa hizi alinyoosha mkono kwetu na kutuambia changamoto za kiafya ni kubwa na la awali ambalo anataka kulifanya ni kuchangia mfuko wa kiafya na changamoto zisiwe gharama za kimatibabu na kutoa dola elfu 20,000, karibu million hamsini," amesema Seba.
Kumbukumbu Muhimu
Utakumbuka August 05, 2017 katika uzinduzi wa Mradi Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya Tanga, Rais Magufuli awalipatanisha Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na tofauti zao kwenye kazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.