ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 1, 2018

WABUNGE MAJIMBO YA NYAMAGANA NA ILEMELA WAUNGANA KUBORESHA MICHEZO.

Afisa Utamaduni Wilaya ya Ilemela Sosho Kizito (kulia) akikabidhi mpira kwa mmoja wa wanafunzi katika juhudi za kuboresha michezo mkoani Mwanza.
Wabunge wa Jimbo la Nyamagana na Ilemela wameahidi kushirikiana na Wadau wa Michezo kuhakikisha wanaboresha na kuimarisha  sekta ya Michezo sambamba na kumaliza changamoto zote zinazoikabili sekta hiyo.
Mhe Stanslaus Mabula.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Mhe Stanslaus Mabula wakati akifungua bonanza la Mchezo wa Mpira wa Kikapu lililoandaliwa na Taasisi ya PSD kwa kushirikisha Shule za Msingi na Sekondari zilizopo mkoani humo kwa lengo la kuibua vipaji na kuukuza mchezo huo, Bonanza lililofanyika katika viwanja vya Nyakabungo kata ya Mirongo jijini Mwanza ambapo amesema kuwa yeye kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wamekuwa wakisaidia sekta hiyo ya Michezo na kuongeza kuwa wataendelea kufanya hivyo ili kuboresha sekta hiyo sambamba na kuahidi kutafuta Wadhamini wa kuunga mkono maandalizi ya mashindano makubwa ya mpira wa kikapu nchini yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo mapema Disemba, 2018.

‘… Mimi na mwenzangu mbunge wa jimbo la Ilemela tunaahidi kuendelea kushirikiana na nyinyi kuhakikisha tunaboresha sekta hii ya michezo, Na mara zote tumekuwa tukifanya hivyo …’ Alisema


Kwa upande wake Muwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni katibu wa mbunge huyo kwa Kanda ya Bugogwa, Bi Rebeca Anael Yusuph amesema kuwa Dkt Angeline Mabula amekuwa mdau mkubwa wa mpira wa kikapu kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili mchezo huo sambamba na kushika nafasi za Uongozi ikiwemo mwenyekiti wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza na Mweka Hazina wa Chama hicho Taifa mbali na kuwa mchezaji wa mpira huo kwa Timu ya Taifa huku akiwaomba wadau wa maendeleo kushirikiana na viongozi wa majimbo hayo kuifanya sekta hiyo kuwa ajira rasmi kwa vijana.

Nae mratibu wa Bonanza hilo ambae pia ni Afisa Michezo wa manispaa ya Ilemela Ndugu Kizito Bahati Sosho mbali na kuwashukuru wabunge wa jimbo ya Nyamagana na Ilemela kwa msaada wao katika kusaidia mchezo huo, ametaja mafanikio waliyoyapata kupitia sekta hiyo ikiwemo kuibua vipaji kwa kuzalisha wachezaji wanaotumika na Timu ya Taifa na Virabu vikubwa nchini sambamba na kuwaomba kufadhili mashindano makubwa yatakayofanyika mkoa wa Mwanza mwishoni mwa mwaka huu.

Katika Bonanza hilo Timu za kutoka Shule ya Bwiru wasichana, Bwiru wavulana, Joseph & Mary, Mesa, Kiloleli, Kilimani, JMond, Nganza, na nyenginezo nyingi  zilichuana vikali na hatimae Timu ya JMond kuibuka mshindi wa jumla.






Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.