Macedonia imeshindwa kubadilisha jina la nchi hiyo na kuitwa Macedonia ya Kaskazini baada ya kura zilizopigwa katika maeneo mengi kukataa kitendo hicho.
Kura hizo zimekua pungufu ya asilimia 50 ambazo zilikua zikihitajika ili kuweza kufanikisha suala hilo, hii ikitajwa kuchagizwa na kampeni zilizofanywa na wanaharakati wa upinzani kupinga jambo hilo.
Jina ambalo lilipendekezwa lilikua ni kwa ajili ya kumaliza mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa dhidi ya nchi ya Ugiriki, ambayo imeifanya Macedonia kushindwa kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya sambamba na NATO.
Waziri Mkuu wa Macedonia Zoran Zaev amahidi kwamba ataendelea na juhudi zake za kulibadili jina rasmi la taifa hilo.
Matokeo hayo yazirudisha nyuma jitihada za waziri mkuu wa Macedonia Zoran Zaev, ambaye alilitaja suala hili kuwa ajenda yake kuu.
Wanaounga mkono kutokubadilika kwa jina la nchi hii wamefanya mkutano mkubwa nje ya jengo la bunge kwenye mji mkuu Skopje.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.